ATEKETEA KWA MOTO AKIWA GESTI

0


 

MTU mmoja mkoani Kagera aliyetajwa kwa jina la Neema Bayo (49) aliyekuwa ndani ya moja ya vyumba vya nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Anti iliyoko wilayani Muleba mkoani Kagera amepoteza maisha kwa kuteketea kwa moto ulioteketeza nyumba hiyo ambao hadi sasa chanzo chake hakijajulikana baada ya kushindwa kujiokoa.

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Kamishina Msaidizi, Revocatus Malimi alifika kwenye eneo la tukio na kupata maelezo ya awali kutoka kwa mhudumu wa hoteli hiyo.

 

Baada ya kupata maelezo hayo akielezea juu ya tukio hilo amesema kuwa marehemu huyo alikuwa ni mmoja wa watu watano walikuwa wamefikia kwenye nyumba hiyo ya wageni ambao walinusurika kifo baada ya kujiokoa kufuatia moto huo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top