ALIYENYIMWA UNYUMBA ADAIWA KUMUA MKEWE!

0


 

Fausta Silayo (22), Mkazi wa Kijiji cha Samanga wilayani  Rombo ameuawa kwa kuchomwa kisu na mume wake kwa madai ya kumnyima unyumba.


Mwanamke huyo ambaye bado alikuwa uzazi wa mwezi mmoja alichomwa kisu Julai 23 na kupelekea kifo chake Julai 24 wakati alipokuwa amewahishwa Hospitali ya Huruma kwa ajili ya matibabu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwanamke huyo ambao amesema baada ya mwanaume huyo kufanya tukio hilo alikimbilia nchi jirani.


"Jeshi la polisi linaendelea na jitihada za kumtafuta mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye inasemekana amekimbilia nchi jirani ili kumkamata na kumchukulia hatua za kisheria,"amesema Kamanda Maigwa.


Kamanda Maigwa amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma ya Mkuu kwa maandalizi ya mazishi baada ya taratibu za uchunguzi kukamilika

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top