AVAMIA NYUMBA NA KUNYAKUA MTOTO,WENGINE WAJERUHIWA

0


Huko katika Kijiji cha Kangeme kata ya Zugimlole Kaliua mkoani Tabora Majira ya saa 9 usiku Fisi alivamia makazi ya watu na kumnyakua mtoto wa mwaka mmoja na nusu na kukimbia nae kisha alimjeruhi vibaya na kusababisha kifo chake.


Baadae wananchi watatu walijeruhiwa vibaya na fisi huyo walipojaribu kupambana nae na mmoja kati yao hali yake ni mbaya na amelazwa hospitali ya rufaa ya mkoa Kitete.


Akisimulia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi SAFIA JONGO amesema askari walipofika kwenye eneo la tukio fisi huyo alijaribu kuwashambulia maafisa hao.


"Naomba niwatanie watani wangu wanyamwezi, risasi 49 zimepotea kumuua fisi, sasa huyo ni fisi au fisi wakinyamwezi?" Kamanda Jongo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top