AVIMBA SEHEMU ZA SIRI BAADA YA KUPAKUA ASALI YA MKE WA MGANGA WA JADI

0

 


Kijogoo mmoja kutoka mtaani Kabiria, Nairobi nchini Kenya amelazimika kujifungia chumbani kwa siku saba bila kuona jua baada ya sehemu zake za siri kurefuka na kufura alipochepuka na mke wa mganga wa kienyeji.

Inaarifiwa kwamba jamaa alijua kwamba jirani yake aliyekuwa mganga na wake wanane hangeweza kuwahudumia wote naye akajitolea kumsaidia. 

“Ni mzee sana. Gemu ya wanane haiwezi! Yatushinda sisi vijana sembuse mzee asiye na meno?” jamaa alijisifu jinsi alivyonukuliwa na Taifa Leo. 

Penyenye zinasema kwamba mpiga ramli huyo alikuwa kipofu jombi alianza kuchezea mechi nyumbani kwa mganga huyo bila aibu. 

Asali ilikuwa tamu kwa kuwa hata baada ya kuonywa, lofa alizidi kuipakua kila alipotaka.

 Hata hivyo siku ya kioja ilipofika, baada ya jamaa kurina asali ya mke wa mganga alishindwa kuvalia suruali kwani sehemu zake za siri zilivimba zikajaa na kujaza suruali kupindukia. 

Ilimbidi aende kwake usiku akiwa amejifunga leso ya mke wa mganga huyo. “Jamani nala kiburi na ujeuri wangu. Kipi nilichovuna kwa mke wa mtu isipokuwa haya maradhi yasiyo ya kawaida,” lofa alilia.

Duru zinaarifu kwamba jamaa alikimbizwa katika hospitali zote lakini madaktari wakasema wasingeweza kuutibu ugonjwa wake.

 Jamaa alianza kujuta na kuamua kwenda kwa mpiga ramli kukiri makosa yake na kuomba msamaha ili amgangue apone.

 “Nafa! Nitaenda kuomba msamaha kwa jirani yangu,” jamaa alisema akielekea kwa mganga ambaye inasemekana alikuwa akimsubiri. 

“Mimi nimekusamehe na ugongwa huu uishe. Hata hivyo lazima unihakikishie kwamba hautamgusa mke wangu siku nyingine tena! Wake zangu wote ni waya ya stima ukikanyaga nawe utalia,” mganga alisikika akimuonya jamaa huku wawili hao wakikumbatiana. 

“Ukitamani mke wangu, njoo uniombe ruhusa kwanza,” mpiga ramli alimweleza kwa kejeli kijogoo. Jamaa alirejea kwake akiwa mzima na mwenye afya baada ya mganga huyo kumnasua kutoa kwenye ndumba yake.

Chanzo - Tuko News
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top