BABA ATUHUMIWA KUMUUA MWANAE KWA KUMKATA NA PANGA

0

 


#HABARI  JESHI la Polisi mkoani Rukwa linamsaka, Allon Simfukwe, mkazi wa Kitongoji cha Kaloleni Manispaa ya Sumbawanga kwa tuhuma za kumuua mtoto wake Kadius Allon (3), kwa kumkata na panga.

 SOMA Simulizi sehemu ya 1&2
NATAMANI NIFE LAKINI BADO SIJAITWA BABA


Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, William Mwampaghale, amesema mtuhumiwa huyo anadaiwa kumuua mtoto wake kwa kumpiga na panga, kwamba tukio hilo lilitokea Julai mosi, mwaka huu katika Kitongoji cha Kaloleni.


Amesema Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta ili achukuliwe hatua za kisheria.


Inaelezwa kwamba licha ya kudaiwa kutekeleza tukio hilo, Simfukwe amekuwa akitoa lugha za vitisho kwa Mwenyekiti wa Mtaa.


Inadaiwa kuwa kabla ya Simfukwe kufanya mauaji hayo alikuwa na mgogoro wa kifamilia na mkewe uliosababisha mwanamke huyo kukimbilia nyumbani kwao na kumuacha mtoto huyo akiwa na baba yake.


#via_nipashe

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top