MTU mmoja ambae jina lake halijatambulika amefariki dunia kwenye vurugu zilizo tokea baada ya mtu huyo kufika na chuma cha kupondea mawe maarufu kama (moko ama sululu) na kumshambulia askari mmoja wa Usalama Barabarani akiwa kazini na wenzake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, amesema tukio hilo limetokea leo majira ya saa 3, asubuhi katika barabara ya Ushirombo Katoro wilaya ya Geita inadaiwa kwamba mtu huyo mwenye jinsia ya kiume aliwavamia askari hao na kumjeruhi askari mmoja H.1619 PC JOHN kwenye taya na kidevuni na kumsababishia majeraha.
Baada ya mtu huyo kumjeruhi askari, askari mwingine aliekuwepo alimdhibiti lakini alizidi kumtishia na kutaka kuwajeruhi maaskari wote walio kuwepo wananchi walisogea eneo la tukio na kuwasaidia Askari kumdhibiti mtu yule akaanza Kukimbia wananchi walimponda mawe na kumwangusha chini.
Kamanda amesema Askari na huyo mtu walipelekwa Kituo cha Afya Katoro kutibiwa akiwa chini ulinzi mtu huyo alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.
Soma hii >>MBOWE APINGWA NA WANANCHI