SIMULIZI; NATAMANI NIFE LAKINI BADO SIJAITWA BABA~~~SEHEMU YA PILI

0

 


Leo tunaendelea sehemu ya pili...simulizi hii hhaki miliki ni Iddi Makengo fuatilia kupitia Facebook page Iddi Makengo. 

Inaendelea........

Kitu kilipiga “Paaap!” Kwenye moyo wangu nilikua na hasira kidogo lakini kuna namna falani ni kama nilikua najisikia raha tena sana. Muda mrefu ulikua umepita bila kuwasilianan na Salma, nilkikua nishaanza kumsahau ingawa mara moja moja nilikua nikimkumbuka huku nikiwaza “Hivi kwanini aliniacha?”

SOMA HAPA SEHEMU YA KWANZA...

        <<<<CLICK HERE CLICK HERE >>>>

“Kumbe bado ananipenda, yaani mpaka kuchunguza kuwa nina mwanamke mwingine itakua ananifuatilia na amenikumbuka, aisee! Nataka anayeye aumie kama nilivyoumia mimi!” Niliwaza huku nikitabasamu. Jackline (Sio jina lake halisi) aliniangalia kwa mshangao kidogho kwani sisi hatukua wapenzi na hakuna hata simu moja nilishawahi kumuambia kuhusu mimi kuwa wkenye mahusiano.


Mara nyingi kila alipokua akiniuliza kuhusu mahusiano nilikua nabadilisha mada na kujifanya kama sijamsikia vizuri.

“Ni nani huyo ambaye anataka kuniua kwaajili yako? G, nawewe una siri, yaani unataka kuniambia nina wifi yangu huko lakini simjui? Nitambulishe bwana, mimi sitaki mambo ya kuja kupigwa huko mtaani kwasababu yako…” aliongea kwa utani, nilimuambia hakuna kitu ni mtu tu nilikua naye lakini si ishu siriasi.


“Sikujua hata ananipenda kiasi hiki mpaka kufikia kukufuatilia, usijali nitaongea naye na nitemuelezea kuhusu wewe, sitaki aje kukusumbua.” Nilimuambia kwa mkato, hata alipotaka kumjua huyo mwanamke sikua na chakumuambia, kusema ukweli nilimtamani kujisifia mbele yake, kumuambia kuwa ni mwanamke wengi, niko naye na tunampenda, ana wivu sana lakini bado nilikua sijawa na uhakika ni kwanini Salma aliamua kumtafuta rafiki yangu na kumpa vitisho kana kwamba ni mwanamke wangu.


Nilijiaminisha kuwa nishaachana naye na sina mpango naye kabisa, lakini katika kipindi chote cha mahusiano hakuna siku niliyojisikia vuzuri na kijisikia kama mwanaume zaidi ya siku ile.  Ilikua ni mara yangu ya kwanza kugombaniwa na mwanamke, aisee nilisikia raha. Mara nyingi wakati mimi nasumbuliwa, namfumania mwanamke wangu na kunifanyia vituko vingi nilikua nikisikia rafiki zangu wakiwaongelea wanawake zao


Namna walivyokua wakibadilisha wanawake, kufumaniwa na wao kuombwa msamaha ilikua inaniumiza sana kiasi kwamba nilikua sijioni kama mwanaume.

“Atakua bado ananipenda na hata afanye nini siwezi kurudiana naye, nilikua tayari kubadilisha mpaka dini kwa ajili yake akaniacha tena kwa kunidhalilisha halafu leo ananifuatilia, hapana, akinitafuta na kuniambia kuwa anataka turudiane basi namtukanawee kisha namuambia kuwa sikutaki nina mtu wangu! Tena huyuhuyu Jack ndiyo atanisaidia, aisee, lazima ajue kuwa na mimi ni mwanaume aliniona wanini, basi mimi naanza kumuona wa kazi gani!”


Nilijiambia mwenyewe huku bado nikitabasamu, Jack alikua akiniangalia nikiwaza mwenyewe, aliniangalia nayeye akacheka.

“Unajua wewe ni mwehu, yaani mwenzako natishwa ila wewe unacheka!” Aliniambia kwa utani huku akinipiga kakofi kauso kama kakimapenzi hivi.

“Hahahahaha…. Hapana bwana, sijacheka, nimeshangaa tu mambo yenu wanawake, mnakuaga na wivu mwingine wa ajabu… hata hakuna kitu, nitaongea naye, mtu mwenyewe si kama niko naye siriasi kihivyo lakini anapanini kuniona niko na wewe!”


Niliongea huku nimkimshika na kumkumbatia Jack kwa nyuma, yaye alikua ni mfupi kwangu hivyo nilimshika kwa nyuma nikamkumbatia kama nainama huko makalio yake  makubwa yakihangaika na mwili wangu, alikua ni mzuri, kila siku nilimuona kama ni mzuri lakini hakuna hata siku moja nilishawahi kumtamani. Mara zote nikiwa naye hata akikaa vibaya nilikua nikimuona kama mwanaume mwenzangu, hata kusisimkwa nilikua sisisimkwi.


Lakini siku hiyo ni kama nilikua nimerudishiwa uanaume wangu. Nikiwa nimemshika nilijikuta nasisimkwa mpaka uume wangu kusimama, aliusikia na makusudi alijitingisha tingisha kama vile anajiondoa mikononi mwangu lakini sikumpa hiyo nafasi.

“Unataka kufanya nini wewe?”  Aliuliza kwa hasira kidogo kwani ni kama nilizidisha kumshika kwa nguvu hivyo akashtuka labda ninataka kumfanyia kitu kibaya.


Hapo ndipo na mimi nilishtuka na kujua kuwa nishaharibu

“Hakuna kitu bwana, nimekushika tu nikajikuta imekua hivyo.” Nilimuambia huku nikijitoa kwake kwa aibu.

“Mimi sitaki mambo yako, yaani ndiyo tumetoka kuongea kuhusu mwanamke wako halafu unanishika, hivi wanaume mkoje, kwahiyo sikuzote huniambii chochote leo najua una mwanamke ndiyo unajifanya kama unanipenda?”


Aliniuliza, nilikua sijamuambia kama nampenda lakini yeye ni kama alishajiongeze, hali hiyo ilinifanya kujisikia vizuri zaidi, kawivu alikokua ananionyesha na hasa namna alivyokua ananiongeolea kana kwamba mimi ni malaya ilinifanya kuzidi kuchanganyikiwa zaidi. nilihisi kama na mimi nagombaniwa na wanawake wawili.

“Kwahiyo uansemaje? Umekasirika?” Bila kujijua nilijikuta nimejibu kwa sauri ya juu iliyokua imejaa kadharau flani. Ni kama vile alikua ni mpenzi wangu amenifumania amekasirika.


Aliniangalia kwa hasira na kunisukuma pembeni.

“Wanaume wote kumbe Mbwa tu, hata wewe nilijua mstaarabu kumbe walewale!” Aliongea kwa hasira na kutoka zake nnje, sikumfauata wala kujaribu kumuuliza kitu chochote. Kwangu kugombaniwa na wanawake wawili ilikua ni hatua kubwa sana, nilijihisi furahaa nikawa sasa nasubiria simu ya Salma, nilijua kuwa lazima kuna kitu ambacho si sawa huko kwake ndiyo maana kaamua kumtafuta Jack akiamini kuwa ni mepnezi wangu. Niliamini kuwa labda ananipenda na atakuja kunitafuta tu, sikutaka kumtafuta nilitaka yeye ndiyo aanze kunitafuta.


*****


Furaha yangu haikudumu kwa muda mrefu, nikiwa naamini kabisa kuwa Salma ananifuatilia ndiyo maana amemtafuta Jack, nikiwa naamini kuwa labda atarudi kwangu atannitafuta yeye mwenyewe wiki ilipita bila kiusikia simu yake. Ni kitu ambcho nilikua ninakingojea kama mfanyakazi anavyosubiria msharaa mwisho wa mwezi, kila dakika kuangalia kwenye simu yake kama meseji ya muamala imeingia.


Sikutaka kuanza kumpigia ingawa namba yake nilikua nayo kichwani, nilitaka anitafute yeye ili nimjibu vibaya na kumuambia kuwa sitakia anisumbue mimi nina mtu wangu nampenda sana. Kichwani nilikua nikiamini kuwa huko aliko mambo si sawa, wiki nzima nilikua nikiiangalia simu kila dakika, wiki nzima nilikau situlii, sina amani lakini huwezi amini hakunitafuta. Raha yote niliyokua nayo iliyeyuka, kila kitu kilibadilika, nikajikuta nakua na hasira basi mimi ndiyo nikaanza kumfuatilia.


Nilifuatilia nikaja kujua kuwa alikua bado alikua akiishi na yule mwanaume wake,  Biashara ilishakua kubwa na huyo mwanaume ndiyoa likua akiisimamia, niliuliza kuwa mbali na huyo mwanaume aliyekua naye alikua na mwanaume mwingine ambaye kipindi hicho alikua ni mbunge tena maarufu sana, ni mara kibao alikua akienda Dodoma na huyo mwanaume, mbali na huyo alikua na wanaume wengine wawwili, mmoja alikua ni Dereva Bajaji na  mwingine alikua ni mume wa rafiki yake.


Nikisema rafiki yake namaanisha ni rafiki yake damudamu, yaani walee wapika na pakua. Rafiki yake ambaye hata kipindi ananiacha nilijaribu kumtafuta ili kujua shida ni nini kaanz akunitukana namna nilivyokua nikimnyanyasa rafiki yake na kuniambia nimuache na maisha yake. Alikua akitembea na mume wake tena mara nyingi akisafiri anaenda kulala mpaka kwa huyo rafiki yake.


“Sasa kama ana wanaume wote hawa kwanini anahangaika na mimi? Anashida gani huyu mshenzi?” Nilijiulzia lakini sikupata majibu.  Baada ya kuona  kuwa hanitafuti na hahangaiki na mimi basi niliamua kumuonyesha kwua na mimi nilikua na furaha, sina mpango na yeye na mimi nina maisha yangu.


Tangu kutokea kwa lile tukio nilikua bado sijaongea na Jack, tulikua tunakutana ofisini lakini nikimsalimia alikua anajifanya kutokusikia na kama tunakua mbele za watu basia taitiokia kidogo tui kwa shingo upanda. Baada ya kuona kwua kule mambo hayendi vizuri niliamua kumtafuta, nikaomba kuongea naye, ni kama naye alikua anasubiri nimtafute, ni kama alinimisi kwania linipa nafasi ya kuongea naye.


Nilimuomba msamaha na kuamua kumuambia kuhusu mahusiano yetu ya nyuma. Sikumuambia kama niliachwa na mwanamke akanidhalilisha, hapana, nilimuambiambia kuwa nilikua naishi na huyo wmanamke, namlelea mtoto wake lakini nilikuja kuachana naye kwasababu ya dini.


“Wakati nakutana naye alikua na ujauzito wa mwanaume mwingine, mimi nilimsaidia kama rafiki kwakua tangu mwanzo nilijua kuwa yeye ni muislamu na mimi nilishaapa kuwa siwezi kuoa muisalamu.lakini kwa jinsi tulivyokua karibu bila kujijua tukaingia kwenye mahusiano, ile kujakuja kwangu tukazama, aliniambia kuwa atakubadili kubadilisha dini na kwelia likua tayari kwa hilo.


Lakini yalipokuja masuala ya nyumbani, kwao waligoma kabisa asibadilishe dini, kuona hivyo namimi nikaona hakuna namna kwani mbali ya kwamba mimi mwenyewe sikua tayari kuao muislamu lakini nyumbani nako waligoma. Hapo nikampa mtaji na kumuambia tuachane, naona bado hajanisaidau kwani ni karibu miaka miwili sasa ila bado ananisumbua. Siko kwenye mahusiano nayeye na niko karibu nawewe kwakua unanivuria ila sikutaka kukurupuka nilitaka tujuaje vizuri kwanza.”


Nilimuambia, ulikua ni uongo lakinia mbao uliendana kidogo na ukweli, nilijua kama ningemdanganya sana ipo sikua ngegundua kuwa nilishawahi kuishi na mwanamke na ingekua shida. Alinisikia na kunielewa ila bado alikua na hasira, nilimuombakumtoa out siku hiyo ili tukaongee vizuri na kweli alikubali.


Kusema kweli sikua na mpango kabisa wa kutoka naye lakini nilishachunguza ratiba ya Salma, sehemua bazo anapenda kwenda hivyo nilitaka kutoka naye nikiamini kuwa hata kama asipo9niona yeye, watu hao hao aliowatumia mpaka kujua kuwa nipo na Jack, akapata wivu angewatumia kuchunguz anajujua kuwa siku ile nilitoka naye. Nilitaka sana ajue kuwa nina maisha yangu na sihangaiki tena nayeye. Ukweli nikuwa nilikua naumia na nilitaka kwenda kila sehemu ambayo niliambiwa kuwa huwa anaendaga.


Nilihangaika sana kutoka na Jack karibu kila siku lakini hakuna hata siku moja ambayo nilikutana na Salama, hali hiyo ilizidi kiniumiza. Ni kama alikua na maisha yake mengine na hana shida na mimi. “Lakini kwanini alimtafuta, kwanini anakumbushia maumivu?” Nilijiuliza bila majibu. Baada ya kuona hanitafuti na wala sikutani naye niliamua kuanzisha mahusiano rasmi na Jack, tulishakua marafiki kwa muda mrefu na niliona kumbe nayeye alikua akinipenda, nilianzisha mahusiano rasmi huku nikilazimishia kuwa nataka kuzaa naye.


Sijui kanini lakini bado maneno ya kuwa siwezi kumpa mwanamke ujauzito yaliniingia kichwani nilitaka kuwa na mtoto ili kuuonyesha ulimwengu mzima kuwa mimi ni kidume. Jack alikua akinijua, nilikua rafiki yake na alikua anapenda kuwa na mimi, nilipomuambia suala la mtoto aliniambia hawezi kubeba mimba yangu mpaka nijitambulishe kwao.


“Hakuna shida, kama ni kukuchunguza nilishakuchunguza sana hivyo naamini wewe ndiyo utakua mke wangu. Nilienda kujitambulisha kwao mimi kama mimi huku tukipanga namna ambavyo nitatuma watu. Nilikua na wasiwasi sana nikamuambia kuwa nahitaji mtoto kwanza kabla ya chochote, hata yeye ni kitu alichokua akikitaka sana. Alibeba ujauzito wangu, kusema kweli sikuamini kwani kila siku nilishajua kuwa sina uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito laklini tulipojaribu siku moja tu mimba ailiingia.


Alipima kwanza kwa kipimo cha haraka kisha kwenda hospitalini kabisa, baada tu ya kuhakikisha kweli ana mimba nilijikuta naanza kutangaza. Mara napost picha Mama kijacho, mara nampenda na kila kitu nikitaka ulimwengu kuona kuwa nimeweza kumpam mwanamke ujauzito.


“Hongwara naona unaenda kuwa Baba….” Siku moja usiku wa manane simu yangu iliita, ilikua ni namba mpya lakini nilipopokea sauti ilikua ni ya Salma. Ni simu ambayonilikua naisubiria kwa muda mrefu, karibu ya kila kitu nilichokua nikikifanya nilifanya kwaajili yake, nilitaka kumuonyesha kuwa mimi ni kidume!


“Nashukuru, mambo ya kawaida sana hatyyo….” Nilimuambia kwa kujishaua nikiona kama namuumiza.

“Huyo mwanamke naye ana moyo, ndiyo kaamua kukuzalia… Hahahahahaha hahhahahahah…” aliniambia kwa dharaau, nilijua kaumia hivyo na mimi nikataka kumchoma.

“Wewe si ulishindwa ukaanza kunitangaza kuwa siwezi kuzalisha mwanam ke, sasa ndiyo hivyo...”


“Ningetaka kuzaa na wewe ningezaa, hivi unajua ni mimba zako ngapi nilizitoa? Asikutaka kuharibu maisha yangu kwa kuwa na mwanaume kama wewe! Huyo dada naye atakua fala tu!” Alijibu kwa hasira na kukata simu, ingawa niliumia kuwa alikua anatoa mimba zangu lakini sikujali sana, nilimpotezea kama siku mbili hivi bila kumtafuta huku nikiendelea kupost picha zangu nikiwa na Jack.


Siku ya nne hivi jioni Salma alinipigia simu, aliniambia kuwa anataka kuonana na mimi hivyo anaomba kuja kwangu. Nilimkatalia sana na kumuambia kuwasimhitaji lakinia likazania, nikiwa sina hili wala lile huyu hapa mlangoni, alianza kugonga kwa fujo huku akilazimishia kuingia, ili kukwepa kudhalilika nilimfungulia mlango.


“Unafikiri unaweza kuniacha kirahisi namna hiyo, yaani hivi hivi tu uende kuwa na mwanamke mwingine, hapana!” Aliongea huikua kilia, nilihisi kama ni machozi ya uongo lakini yalikua ni ya kweli.

“Huwezi kuoa mwanamke mwingine, mimi bado nakupenda, nilifanya makosa kuachana na wewe, yaani bora kufa kuliko kukuona ukiwa na mwanamke mwingine!” Alizidi kuongea, nilimshika na kutaka kumtoa nnje lakini hakuataka kabisa, sijui alikua na nini ila ni kama mimi ndiyo nilikua nimemkosea.


“Wewe si una mwanaume wako, si unaishi na mwanaume, si unatembea na mbunge, si uinatembe na flani na flani….” Alishtuka kidogo kuona kuwa najua mambo yake lakini hakujali sana, aliniambia kuwa bado ananipenda na hawezi kuniacha.

“Najua nilikukosea ila unatakiwa kunisamehe, sina furaha kabisa, sidhani kama naweza kupata mwanaume kama wewwe, najua hata wewe unanipenda, nataka unipe muda niachane na kila mtu nije tuishi wote, nahitaji kufanya mapenzi na wewe, nipo kwenye siku zangi za hatari na nitabeba mimba yako!”


Aliongea mambo mengi kwa wakati mmoja, mimi kwangu ilikua ni sherehe, kilikua ni kisasi ambacho nilikisubiri kwa muda mrefu sana, sikua na mpango naye kabisa nilifurahi kuwa kumbe bado ananipenda.

Namuacha kila mtu nataka uwe mume wangu, nipo tayari kubadilisha dini kwaajili yako mwanangu anakupenda sana mpaka leo anakuulizia!” Aliniambia lakini sikua tayari kuendelea naye, nilimuambia simtaki, nikamshika na kutaka kumtoa nnje kwa nguvu.


Alinisihi sana lakini niligoma, nilimuambia nina mtu wangu, nishajitambulisha kwao hivyo siwezi kumsaliti kwaajili yake yeye aendelee na maisha yake tu.

“Basia cha nichukue Pochi yangu, huna haja ya kunitoa kihivyo ngoja nitoke mwenyewe….” Aliniambia, nilimuachaia akahcukua Pochi yake, alitembea mpaka mlangoni ile kufika tu nilishangaa kafungua Pochi, akatoa kisu kikubwa na kuitupa Pochi pembeni.


“Kama hutaki kuwa na mimi ni bora kufa, nife mnimi au ufe wewe ila sitaki kuachana na wewe. Huwezi kuniacha nakupenda sana….” Alichukua kilam kisi na kutishia kujuia.

“Siwezi kuishi bila wewe na ukiniacha najiua. Nikiwa sina hili wala lile alinyanyua kile kisu kweli na kujichoma tumboni, Damu zilianza kumwagika kimasiharaa masihara niliona kama anakufa mbele yangu.


Je, salama ndiyo Baibai au itakuaje, vipi Jack akisikia atafanya nini, usijali.


ITAENDELEA…..

Kupata mwendelezo fuatilia ukurasa was Facebook wa Iddi Makengo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top