Niko kwenye mahusiano kwa mwaka mmoja sasa, kuna Dada niko naye, ananipenda sana na mimi nampenda sana. Shida inakuja kuwa mimi nayeye dini ni tofauti, yeye kakataa katakata kubadilisha dini ila yuko tayari kufunga ndoa ya kiserikali.
Nampenda sana kwani pamoja na yote lakini naye ananipenda tena sana. Sababu ya kuja kwako ni hivi, mwaka jana kutokana na suala la dini tuliamua kutafuta mtoto, sasa katika hangaika hangaika ikashindikana tukaamua kupima, yeye akaambiwa kuwa yuko sawa ila shida ni mimi siwezi kumpa mwanamke ujauzito.
Pamoja na kusikia yote hayo lakini alikubali kuendelea na mimi na kwakweli mimi nayeye tunaamani tena sana. Tunaishi pamoja bila ndoa na nataka kufunga ndoa ya kiserikali, lakini shida inakuja kwa ndugu zangu, yaani wameshaanza maneno mpaka natamani hata kufa.
Baada ya kujua tu kuwa ninaishi naye, Mama yangu alikuja na kila kitu chake kuanza kuishi kwangu, haikuishia hapo, kuna binti alikuja naye kama mfanyakazi lakini sasa hivi wananilazimishia kumuoa, kusema kweli nachanganyikiwa kwani naona kama namuumiza sana mchumba wangu.
- Naomba unisaidie, ni kwa namna gani namuondoa Mama yangu hapa nyumbani kwangu. Nimechoka na kelele zao kwani hawajui mambo ninayoyapitia kichwani kwangu, huyu mwanamkea nanivumilia mambo mengi sana lakini nashindwa kuwaambia ndugu zangu kwani nahisi hata hawataniamini na ni maisha yangu.
Nataka kuwa na amani, niishi maisha yangu mbali na ndugu zangu kabisa, mimi ndiyo mtoto wa kwanza wakiume, wengine wote ni wanawake na wanataka mjukuu, najua nikioa wataanza mambo ya mtoto na siwezi kumpa mwanamke ujauzito.
JE UNAPENDA SIMULIZI ZA SAUTI?
BOFYA HAPA KUSIKILIZA/DOWNLOAD FREE
Pia kuna dawa natumia na huyu mchumba wangu ananisaidia sana kuniweka sawa kiakili lakini hawa ndugu zangu naona wanazidi kunichanganya. Mama yangu anaonega sana, anapenda kumtukana mchumba wangu tena makusudi, kuna wakati nakasirika natamani hata kumpiga kwani anafanya mbele yangu ila mchumba wangu ananizuia, nisaidie nifanyeje kwani huyu dada akiniacha sijui nitafanya nini?