Mtu Mmoja Aliyejulikana Kwa Jina La Edita Mangita (40) Mkazi Wa Mtaa Wa Matema Kata Ya Maguvani Mkoani Njombe Amefariki Dunia Baada Ya Kujifungia Na Jiko La Mkaa Katika Kibanda Chake Cha Kufanyia Biasahara.
Kwa Mujibu Wa Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Njombe Hamisi Issah Tukio Hilo Limetokea Julai 28, 2021 Ambapo Marehemu Edita Aliamua Kubaki Na Kulala Katika Kibada Chake Cha Biashara Ili Kuwahi Wateja Wake Wa Asubuhi.
Aidha Kamanda Issah Amewataka Wananchi Wa Mmkoa Wa Njombe Kuacha Kulala na Majiko Ya Mkaa Ndani Huku Akitoa Wito Kwa Wataalamu Wa Afya Kuendelea Kutoa Elimu Kuhusu Madhara Hayo Ili Kuiokoa Jamii.
Kamanda Issah Ametaja Tukio Lingine La Mwanamke Mmoja Imelda Mgeni Ametelekeza Mtoto Mwenye Umri Wa Miezi Mitatu Kwa Mume Wake Naye Kwenda Kusikojulikana.
Credit-Kingsfm