Huyo Baba na huyo Mama unayemuona hapo ni watu walioishi kama mke na mume na walibahatika kupata watoto wawili kwa hakika maisha yalikuwa mazuri huyo Baba alikuwa na kazi nzuri ambayo alikuwa analipwa mshahara mkubwa sana hivyo akaona amtafutie kazi mke wake ili wawe wanapata pesa huku na huku wasomeshe watoto pia wasihishi kwa kutegemea kazi moja tu.
Kwa kuwa mwanaume alikuwa na uwezo na kujuana na kampuni mbali mbali alifanikiwa kumtafutia kazi mke wake kwenye kampuni nyengine hivyo wakawa wanapata pesa huku na huku, baadae maisha yalikuwa mazuri watoto walikuwa hawajuhi shida na walikuwa wanasoma shule ya hadhi ya juu.
Maisha yaliendelea ila kwa bahati mbaya baadae upepo ambao sio mzuri ulipita kwao kule kazini kwa mwanaume kulitokea wizi wa fedha nyingi sana mpaka kampuni kuyumba hivyo kwa kuwa yeye alikuwa ngazi ya juu pale ofisini akafukuzwa kazi ilionekana kama yeye ndo kaiba hizo fedha.
Maisha yaliaanza kuwa magumu kwa kutegemea kipato kimoja ile nyumba aliyokuwa anaishi na familia yake haikuwa yake alipangishiwa na kampuni hivyo basi nyumba pia alinyang'anywa, hali ilizidi kuwa ngumu mpaka ilipelekea watoto kufukuzwa shule kutokana na kukosa kulipiwa ada, wakaamishwa zile shule wakizokuwa wanasoma awali na kupelekwa shule kata.
Kadri mda ulivyokuwa unazidi kwenda mwanamke akaanza manyanyaso kwa mme wake mara hasimpe haki yake ya ndoa mara amsimange kwa maneno ya kashfa, kuna siku mwanamke alirudi kutoka kazini alimkuta mmewe yupo sebuleni akiangalia TV na wanae alimwambia.
"Hivi wewe mwanamke mzima unaacha kutafuta kazi upo tu nyumbani unabadilsha CD kuangalia muvie inamaana mimi ndo nikulishe na niwasomeshe watoto, hiyo biashara sifanyi nikiona hauangaiki mimi ndo nihangaike peke yangu nitaondoka nitakuachia nyumba ukae na watoto wako halafu tuone mtakula nini mana nimechoka"
Alikuwa anaongea maneno hayo kwa kumfokea huku watoto wakiwa wanasikia kisha akaingia zake chumbani.
Huyo Baba aliwaambia watoto wake "wanangu wala msijali mungu atatusimamia kila kitu kitakuwa sawa tutaishi kama zamani"
Siku zilisonga na Mama alifanya kama alivyotamka alibadilisha laini ya simu akawa hapatikani aliondoka pale nyumbani bila ya kujulikana alipoenda akimuacha mmewe akihangaika na watoto ilifikia hatua hata mlo mmoja kwa siku walikuwa wanakosa ila huyo Baba hakukata tamaa alipambana na watoto wake huku akisali sana kwa mungu asikie kilio chake.
Siku hiyo wakati yupo na watoto wake nyumbani akiwaimbia nyimbo nzuri ya Dini kuwafariji wanae mara ghafla alisikia simu yake inaita kuja kucheki ilikuwa namba ya Boss wake kwenye ile kampun aliyokuwa akifanya kazi awali haraka alipokea wakasalimiana kisha akamwambia.
"Samahani sana ndugu kwa yote yaliyotokea kampuni imepeleleza na kufanya uchunguzi imeonekana wewe hauhusiki na upotevu wa pesa hivyo kampuni imeona ikurudishe kazini na itakulipa pesa ya miezi yote uliokaa nyumbani hivi ninavyokwambia kesho unaitajika uje kazini uanze kazi mara moja"
Huyo baba alifurahi sana mara baada ya kusikia hivyo na aliamini kuwa mungu ndo kila kitu hapa duniani hakuna wa kushindana naye alimshukuru kwa kulia machozi
Kweli alirudi kazini maisha yalibadilika yalirudi kama zamani lakini katika pita pita zake mjini alienda kuwafanyia shopping watoto wake ile anashuka tu kwenye gari kuna Mama alimshika bega lake kwa nyuma alivyogeumka kumbe alikuwa yule mwanamke aliyezaa naye alikuwa amechoka sana akionyesha kama mtu aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu.
Yule Mama alianza kububujikwa na machozi akiomba msamaha kwa kile alichokifanya huku akiwa amepiga magoti.
KWA HAKIKA MUNGU NI MWEMA UKIOMBA ANAJIBU NA USIKATE TAMAA HATA SIKU MOJA IPO SIKU ATAJIBU MAOMBI YAKO.
Type Ameni au Amina, ukishindwa kabisa hata Like tu Mungu atende miujuza katika maisha yako leo.
SHARE HUU UJUMBE UWAFIKIE JAMII NZIMA UPATE BARAKA.
SHARE
SHARE