Mnataka demokrasia, utawala wa sheria na haki, halafu muda huo huo mnamtaka Rais aingilie mahakama akiuke katiba na Sheria za Nchi kwa Maslahi yenu hili halikubaliki kabisa.
Serikali ya Rais Samia itasimamia katiba, sheria, haki na usawa wakati wote bila aibu wala kuyumbishwa, kufanya hivyo ndio chachu ya amani na utulivu nchini,"
Matamshi hayo yametamkwa leo na katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu alipokuwa akitolea ufafanuzi kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kuwa Tanzania iko katika mapambano ya demokrasia ambapo alisema si ajabu na wala si kosa kwa polisi kumkamata kiongozi yeyote wa kisiasa au wa kiserikali ikiwa wataona kuna haja ya kufanya hivyo.
Hii ndio kauli ambayo Shaka ameitumia kuijibu!.
“Tunamtaka Rais amtake DPP afute mashtaka dhidi ya Mhe. Freeman Mbowe.” Mhe. @jjmnyika pic.twitter.com/JgkNDgIvKD
— CHADEMA Tanzania (@ChademaTz) July 31, 2021