Anakusumbua kwasababu humuachi akaona umuhimu wako, kila wakati anakufanyia vituko lakini wewe bado upo. Wanawake wana tabia moja, akishajua kuwa unampenda sana na akahisi kuwa huwezi kumuacha basi anatingisha kiberiti, ataanza kwa vitu vidogo vidogo kuona kama utaongea au utaishia kunyenyekea.
Kwa mfano, ataanza kukujibu kwa dharau au kwa kisirani “Wewe nawe huna akili ndiyo nini sasa… kuwa mtu mzima sasa wewe ni mwanaume… wanaume wenzako hawako hivyo bwana…” Haishii hapo, kuna mamboa mabyo mwanzo alikua anayafanya ataanza kubadiliaka na ukimuuliza anakua mkali.
Mwanzo ulikua unashika simu yake, ila anaweka password na ukiigusa anakuambia sitaki mambo ya kushikiana simu… alikua akienda sehemu anakuaga ila anaanza kukupa taraifa tu au hata hakuambii… baada ya muda anaanza kamtindo, kila mkigombana utasikia “Kama vipi tuachane…” wewe ndiyo unaomba msamaha au kusema yaishe hata kama kakosea yeye.
Kwa mfano akakutukana au kukujibu kwa dharaau, anakuongelesha vibaya mbele za watu usimjibu hapohapo, subiri mko vizuri halafu muambie, “Kuna ule ujinga wako uliufanya jana, nilikua nakuangalia, sitaki, hii ndiyo mara ya mwisho kunijibu kama shoga yako ambaye mnagombania bwana, sina haja ya kukumbusha mimi ni nani ila ukiendelea hivyo tutamalizana sitaki ujinga”
Muambie kisha nyamaza na usizungumzie tena, akirudia usiongee tena, kua mkimya, badiliaka, kama ulizoea kumpigia simu kutwa mara tatu basi acha kupiga, kaa baada ya siku mbili piga, kama ulizoea kumfuatilia kumuulizia mambo yake acha, kujali acha kunyenyekea acha. Kama anakupenda kichwa kitasmkaa sawa na kama hakupendi basi itakua sababu ya kukuacha muambie safari njema.
- Akikuambia “Bora tuachane” kama hujamkosea wewe yeye ndiyo kakukosea mjibu “Umeongea lamaana maana naona kama haya mahusiano yananipa stress tu, kila mtua shike njia yake, nanyuka na ondoka na kama ni kwenye simu muambie siku njema kisha mpotezee…”
Asiporudi kuomba msamaha basi hakua wako, alishakuacha ila akirudi muambie siteki tena huo ujinga na akirudia anza wewe kumuambia tuachane. Ndiyo hata kama unampenda mwanamke vipi usiruhusu akupande kichwani kwani mwanamke aksihajua kuwa huwezi kumuacha basi utateseka, anapaswa kujua kuwa unampenda lakini yeye sio pumzi, unaweza muacha na ukaishi!
NB: Dada zangu kama sauti haitoshi niambieni niongeze!