Kila mara nikikaa na kutafakari juu ya mahusiano/ndoa za zamani na za kisasi hiki kipya cha U bongo Movie nabakia nikiwa nacheka tu huku nikiwa mwenye huzuni.
Leo hii si ndoa za washirika/wasio washirika kila mmoja anapambana na Hali yake katika kuumia, ijapo wengine katika ndoa/mahusiano wanajilaumu kwa nini hawakufahamiana/kujuana mapema, maana wana furaha/Raha/Amani katika Maisha yao.
Hebu tufikirie kwa umakini tofauti ya Ndoa za wazazi wetu na ndoa za Sasa kwa nini za Sasa ni pasua ikiwa tunasema tunaenenda katika Roho? Kwa nini za zamani zilidumu kuliko za Sasa?
NDOA ZA ZAMANI.
Nilpata simulizi kutoka kwa Mzee akisema, kipindi wao wanaoa walikuwa wanatumia wazee kwa kumuangalia binti/kijana anatokea kwenye familia ya namna gani?. Ikiwa Kuna baadhi ya Tabia walijiridhisha Kama Uchoyo, uvivu, magonjwa ya kurithi, tabia za kurithi n.k walikuwa wanaahirisha kumfuatilia mtu huyo na kumtafuta mwingine.
Pia anasema binti wa Enzi hizo alikuwa akiolewa kwa kumfahamu mwanaume sio kumjua, yaani binti alikuwa akiambata na mwoaji bila hata kujua kule anakokwenda atakutana na Nini! Mfano hakuwa anajua watalalia godoro au nyasi, jamvi/ mkeka. Kwa kifupi alienda akitambua mazingira yoyote yupo tayari kuyaishi. Hii iliwafanya wawe wavumilivu Sana.
Pia walikuwa wakioana bila kufunuana nguo(kufanya ngono), kiufupi walioana wote wakiwa mabikra na ilisaidia kuondoa Lugha ya mwenzangu hanifikishi kileleni.
NDOA ZA SASA.
- Ukitazama mfumo unaoendelea kwenye kuanzisha mahusiano unaweza ukaona ni hatari iliyo mbele zaidi japo sio wote. Leo mahusiano yanaanzia Facebook/Social network, Bar/Club/Disco, n.k
Baada ya muda mchakato wa kutambulishana unaanza, mpaka wengine kutoleana posa bila hata kujali suala la kuchunguzana kwa umakini historia ya huyo mtu, mwanzo alikuwaje, kwao ni watu wa Namna gani? N.k
Imefikia mahali watu wanaoana bila kufahamiana, baada ya siku kudhaa unasikia ndoa ya fulani imegeuka kuwa uwanja wa masumbwi ni mtifuano tu. Hii ni aibu!
Leo vijana wengi hawaoani bila kuonjana(kutenda dhambi) kwamba wanahofia kuuziwa mbuzi kwenye gunia kana kwamba wao ni mbuzi. Kizazi HIKI kimejiroga!
Ndugu zangu, Matokeo mengi tunayoyaona leo ni kwa sababu jana tulipanda mbegu nzuri/mbaya. Utaratibu unaoutumia Leo kumpata mwenzi wako ndio Matokeo ya kesho katika Maisha yako ya Ndoa.
Kama leo mnatongazana katika mitandao ya kijamii na mnakubaliana kuishi Pamoja bila kufahamiana, Tambua hata kuvunjika kwa mahusiano itakuwa hivyo hivyo.
Kwa kuwa Ndoa ni mpango sahihi wa Mungu wa Mbinguni kwa watoto wake, ni vyema kuendelea kutembea katika Maelekezo yake Mungu ili akuingize katika kutimiza ahadi yako. Usijifanye wewe unajua Sana kumbe hujui, mwisho wa siku uanze kuwasumbua watumishi wakuombee kwa ujuaji wako.
ASANTE.