KUNA WATU WAOGA KUBEBA KONDOM,SASA BEBENI MKATUMIE WAZIRI ASEMA.

0

 


🎙Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.  Ummy Mwalimu amesema wakati serikali na Jamii ya kitanzania inaendelea kupambana na ugonjwa wa Corona lazima jamii iendelee kuchukua  tahadhari dhidi ya magonjwa mengine ya hatarishi ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI.


Mhe. Ummy ameyasema hayo  Julai 30,2021 jijini Dodoma  alipokuwa anazindua uwekaji wa makasha ya kusambazia kondomu maeneo ya watu na yenye mikusanyiko ambapo ameeleza kwa kufafanua takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka takribani watu  72 elfu wanaambukizwa maambukizi mapya ya ugonjwa huo.


Akiendelea kufafanua  kwa siku watu zaidi  200 wanapata maambukizi  na kuitaka jamii kuendelea kujiepusha  kujikinga na kuendelea  kusikiliza maelekezo na wataalam wa Afya.


Mhe.Ummy alisema jamii iache kuwa na dhana potofu ya ikimuona mtu amebeba kondomu kumuhisi ni muhuni bali jamii ijifunze kujilinda na maambukizi yatokanayo na ngono zembe ambazo zimekua zikiharibu maisha ya baadhi ya watu.


Sambamba na hilo amewaagiza watendaji wa TAMISEMI kwa kushirikiana na Tayoa kuhakikisha wanasambaza makasha hayo na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI hadi maeneo ya Vijijini ambapo baadhi ya jamii haina uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa huo.


Makasha hayo tayari yamefika kwenye halmashauri 169 kati ya halmashauri 184 kwa Tanzania bara hivyo wajitahidi kufikisha maeneo mengi zaidi kuokoa taifa.


Naye  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabil Shekimweli akitoa wito kwa wadau wa maendeleo kuendelea kutoa elimu kwa jamii  athari za ugonjwa wa UKWIMWI na kuwataka kufanya tafiti  ili kujua  usahihi na mahitaji.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top