Mkuu wa Mkoa wa Lindi ametangaza kusitisha shughuli zote zinahusisha msongamano wa watu,ambapo amesema katika kupambana na maambukizi ya Virus vya Corona wananchi wa mkoa huo hawana budi kutekeleza maagizo hayo.
Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telack ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na Mashujaa FM juu ya ugonjwa wa UVIKO-19 July 29, 2021 ambapo amewataka wananchi kutambua kuwa ugonjwa wa UVIKO upo mkoani humo na kupiga marufuku sherehe zote, Disco, na ngoma
Kuhusu wanahitaji kufunga ndoa Mkuu wa mkoa amesema katika ndoa idadi ya watu isizidi wanne huku akiagiza maafisa afya mkoani humo kuhakikisha wasafiri wote wanavaa barakoa, magari hayasimamishi abiria na kuwekwa vitakasa mikono kwa kila chombo cha usafiri.
Pia amepiga marufuku mikusanyiko yote isiyokuwa na umuhimu huku akiagiza shughuli za Minada zinazofanyika kuanzia tarehe moja kila mwezi kusitishwa mpaka wakati mwingine kwa kuwa minada hiyo huchukua idadi kubwa ya watu