Mahabusu sasa kupimwa Covid-19

0

Picha ya Maktaba

 

Serikali imesema ili kuzuia maambukizi ya Covid-19 kuingia magerezani, imeanza kuthibiti vituo vya polisi, magereza na mahakama kwa kuhakikisha tahadhari zinachukuliwa maeneo hayo pamoja na kufanya kipimo cha haraka cha Covid -19 kwa mahabusu wote wanaofikishwa gerezani kwa mara ya kwanza.

Pia imekusudia kutoa kipaumbele cha dhamana kwa mahabusu wenye makosa yanayodhaminika kisheria ili kupunguza msongamano.

Hayo yamesemwa leo Jumapili, Julai 25, 2021 na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi wakati akisoma mwongozo wa udhibiti wa ugonjwa wa corona (uviko-19) kupitia afua ya kuthibiti misongamano katika jamii bila kuathiri shughuli za kiuchumi toleo la kwanza.

“Tumeshaagiza vituo vya Polisi vitatakiwa vinaweka maeneo ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, watumishi na watu wote wanaoingia katika vituo vya polisi wavae barakoa muda wote.

Read more >>>

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top