MAMA SIHOFII KUKATWA MGUU KWANI NAHOFIA KUWAACHA WADOGO ZANGU

0

 


Mwaka wa kumi na moja naishi na mume wangu kwenye ndoa, sijawahi kufurahia ndoa yangu kwa muda mrefu, nakumbuka mume wangu alianza kubadilika nilipokua na ujauzito wa mtoto wangu wa pili. Kwanza shida ilianza katika kufanya tendo la ndoa, alikua hataki kabisa kushirikiana na mimi.


Mwanzo alianza kwa kusema kuwa amechoka hivyo hawezi, baadaye akabadilika na kuwa akisema mimba yangu inamfanya kushindwa kuufurahia mwili wangu, lakini baadaye alihama kabiasa na chumba na kuniambia kuwa, akikaa chumba kimoja na mimi anasikia kichefu chefu na kutamani kuniua.


Ndani ya muda mfupi mume wangu alibadilika, akawa ni mtu wa hasira, kuongea kwa sauri na nilipokua nakaribia kujifungu alianza kunipiga. Alianza kuniambia kuwa mtoto niliyebeba tumboni hakua wake, sijui hicho kitu kilikujakujaje lakini aliku anaanipiga sana huku akiniambia waziwazi kuwa anataka mimba yangu itoke kwani haamini kama mtoto ni wake.


Nakumbuka hata kwenye kujifungua sikujifungua kwa njia ya kawaida, hapana, kwanza alinikataza kabisa kwenda hospitalini, alikua ananiambia hataki kabisa niende hospitalini. Ilikua ni usiku na uchungu ulinishika, nilinyanyuka kwenda kumuamsha mume wangu ambaye alikua chumba cha pembenio akilala na mtoto wetu wa kwanza wakiume.


Nilimuambia kuhusu maumivu na kutaka kujifungua, lakini ghafla tena mbele ya mtotyo alinivamia na kuanza kunipiga, alinipiga san atena sehmu za tumbo huku akinishutumu kuwa namsingizia mtoto na anataka kumuulia tumboni. Sijui ni kitu gani kilitokea kwani alinipiga sana mpaka kuishiw anguvu.


Alinivuruta mpaka chumbani na kunifungia kisha akaondoka, lakini wakati anaondoka nilisikia kama chupa imepasuka, maji yakaanza kumwagika, nilikua kwenye maumivu makali, si ya uchunhu hapana, kwa mtoto wangu wapili sikupata uchungu kabisa. Nikiwa chini nimekaa, nusu fahamu nusu kama sinafahamu mtoto alitoka mwenyewe nikamshika mwenyewe na kitovu hcake nilikata mwenyewe.


Kama masaa mawili hivi nikiwa nimekaa na mwanangu sijiwezi mume wangu alirudi. Alikua ni mtoto wakike lakini kwa maajabu alizaliwa kama kopi ya mume wangu. Yaani tangu kuzaliwa mwanangu alikua ni kopi ya Baba yake, mume wantu akumuona mtoto alianza kulia, alilia sana huku akiomba msamaha akiniambia hajui ni kitu gani kilikua kimemtokea mpaka akawa vile.


Kusema kweli hata mimi nilikua sijui ni kitu gani ambacho kilikua kimempata mume wangu mpaka kubadilika namna ile. Basi alinichukua mpaka hospitalini ambapo nilipatiwa huduma ya kwanza kwani mbali na kujifungua nilikua na maumivu mengine ya mwili. Mtoto alikua salama, alizaliwa na afya nzuri na hakua na tatizo.


Niliruhusia kurudi nyumbani na mambo yalikua mzuri, mume wangu alibadilika, akawa mtu mzuri, ananijali na kunihudumia kwa kila kitu. Hakutaka hata nifanye kazi kwa madai nilee wanae na mimi nilikubali. Lakini amani haikudumu hata kwa miezi sita, miezi mitatu baada ya kujifungua na kwakua nilijifungua kwa njia ya kawaida sikuongezewa hata njia nilipata hamu ya kufanya tendo la ndoa.


Nilimuambia mume wangu akaniambia mtoto bado mdogo, nilijaribu kumshawishi lakini ni kama alikua ananikwepa, aliongea kwa hasira huku akinitukana kuwa mimi ni malaya, nataka kumharibia mtoto wake na maneno kibao. Kwakua tayari nilishaonja raha ya ndoa nilisema hiki si kitu, tendo la ndoa tu nitasubiri, basi nilikaa kimya bila kumuomba tendo la ndoa.


Hapo napo ilikua ni shida, nikikaa kimya analalamika kuwa nina wanaume wengine ambao wananridhisha ndiyo maana simuambii, lakini nikimuambia pia kuwa nahitaji kufanya tendo la ndoa napo alikua nalalamika. Sikumoja nilijikaza nikamuambia, nakumbuka mwanangu alikua na miezi saba, kweli tukafanya lakini mume wangu alikua si yule wa zamani.


Mwanzo tulizoea tukifanya tendo la ndoa anaenda mpaka raundi tatu ila siku hiyo alienda moja tena haikuchukua hata dakika tano. Alilala na kosa nililolifanya ni asubuhio kumuuliza kama kuna tatizo. Alinitukana sana, aliniambia nimebadilika, nimepanuka, nimekua wa ajabu, ninanuka na hatakuja kufanya tena mapenzi na mimi mpaka nibadilike.


“Mbona nikifanya na wanawake wengine nakua vizuri, wewe ni mchawi!” Alinitukana sana na tangu siku hiyo mume wangu alibadika kabisa, alirudia pombe, akarudia kunitukana yaani kila siku ikawa ni kupigwa na kutukanwa. Sikujua mpaka miezi miwili baadaye ndipo nikagundua nina ujauzito mwingine wa mtoto wa tatu, nilimuambia mume wangu lakini kama ilivyokua mwanzo aliniambia kuwa mimba si yake hivyo nitafute Baba mwingine.


Aliniambia kabisa kuwa anataka nitoe, akanipa dawa na kunilazimisha kweli nilikunywa hizo dawa lakini mimba iligoma kutoka. Mume wangu alikua ni mtu wa kukasirika, anachepuka waziwazi, anakuja na wanawake mpaka ndani, ananitukana na mambo kibao. Kutokana na mateso nilijikuta na mimi napandwa na hasira, kila akichelwa kurudi, kila akinitukana au nikipigiwa simu na mwanameke wake basi hasira zangu zilikua zinahamia kwa watoto.


Nilijikuta naanza kuwachukia wanangu, nilijikuta nakua na hasira nikiwapiga wanangu absi ndiyo napata kanafuu, mume wangu akinipiga nakua nasubiri aondoke kisha naanza kuwapiga watoto, nilikua nawapiga sana wanangu tena bila sababu ya msingi. Mara nyingi kila nikimpiga mtoto naishia kumuambia yeye ndiyo sababu, kusema kweli nilikua naona kama wanangu ndiyo sababu ya baba yao kuwa vile, nilikua naona maisha yangu yamebadilika baada ya kuzaa.


Mtoto wangu wapili, ambaye alifanana zaidi na Bqaba yake ndiyo nilikua namuonea sana, nikisema namuonea sijui kama mnanielewa, wakati huo alikua kama na mwaka tu. Ndiyo alikua ni mtoto wa mwaka lakini nilikua nampiga sana kiasi kwamba mtoto wangu mwingine ambaye ni wakwanza, wakati huo akiwa na miaka minne alikua akiingilia kati.


Nakumbuka siku moja mume wangu alirudi kalewa, nilikua nimchoka sana, nimehangaika kupika kwani ilikua ni siku yake ya kuzaliwa, nilimuadnalia Keki na zawadi lakinia lipofika hata hakula wala kujali,a lichofanya ni kunionyesha picha alizokua kapiga kwenye simu yake, zilikua ni picha akifanyiwa shetehe na mwanamke wake akaniambia kuwa mimi sijui kupiga na kaja kubadilisha nguo anarudi.


Aliondoka na kuniacha na ile keki, wakati anaondoka mtoto wangu mdogo wa mwaka mmoja alimkimbilia Baba yake kama anamlilia anataka waondoke worte. Nilijikuta napandwa na hasira, nikasuubiri mpaka Baba yake akaondoka, ile keki ilikua mezani, mtoto alipanda kwenye kiti akaanza kuila ile keki.

“Nahangika mimi halafu anamkimbilia Baba yake huyu shetani atanikoma!” Nilijikuta namvamia mwanagu, nikamsukuma akadondoka chini, mtoto wa mwaka mmoja akadondoka chini kabla ya kumnyanyuka nilianza kumpiga mateke, nilimpiga sana, mtoto wangu wa kiume wa miak amine kuona hivyo, alikimbil;ia mpaka jikoni akaenda akachukua kisu na kunichoma nacho mguuni.


Nilijikuta naishiwa nguvu si kwakua damu zilikua zinanitoka lakini nilijiona kama mjinga kumpiga mtoto wantu namna ile. Lakini pamoja na kujisikia vibaya hata sikumnyanyua, nilikimbilia na kwenda kujifungia chumbani, nakumbuka ilikua ni kama saa mbili za usiku, sikutoka na sikujua nini kimeendelea mpaka asubuhi. Niliamka mume wangua likua bado hajarudi ila wanagu wote wawili walikua wamelala pelepale sebuleni nilipokua nimewaacha.


Nilijisikia vibaya, nikaanza kuwaomba msamaha, nikajionghelesha, niakwapa chakula wakala wkani wlaikua na njaa sana. Siku hiyo nilijiapiza kuwa hata mume wangu anifanye nini kamwe siwezi kuwapiga wanangu. Pamoja na vituko vingi vya mume wangu kweli nilivumilia mpaka nikajifungua mtoto wa tatu, tena salama hospitalini kama wale wengine huyu naye alikua ni kopi ya mume wangu.


Maisha hayakubadilika mume wangua lizidisha wanawake lakini mimi ndani hataki kunigusa kabisa, ilikua shida yaani kupata tendo la ndoa ndani nilikua nalazimika kuomba hata kwa mwezi mzima na anapofanya na mimi basi ni suala la dakika mbili, hakuna cha maandalizi wala nini lakini nilijitahidi kuridhika hivyo hivyo kwani akifanya mapenzi na wewe na usipoonyesha kuridhika basi moja kwa moja ni kipigo.


Maisha yaliendelea hivyo hivyo mpaka nikabeba ujauzito wa mtoto wa nne, huyu alimkubali, sjui kwanini lakini kipindi hiki alibadikika,a kanionyesha upendo ila hata haikudumu kwani mtoto akiwa na miaka miwili nilibeba ujzuito wa mtoto watu wa tano na wamwisho. Hapa ndipo mume wangu alirudia hali yake ya zamani, aliniambia watoto wamekua wengi hivyo nitoe mimba, nilijaribu kufanya hivyo lakini hii pia nayo haikutoka, hata baada ya kuhangaika sana lakini haikutoka hivyo nikalazimika kuzaa.


Nilijifungua bila mfanya kazi, kumbuka hapo nina watoto wanne, ambao hata hawajapishana sana, nilikua naamka ausbuhi kufanya usafi, kumpikia chai, kuwapikia watoto mpaka nalala nakua nimechoka.


Mtoto wangu mdogo alikua anasumbua sana, hataki umuweke chini, akianza kulia huwezi kufanya kitu chochote, usiku mume wangu haamki kabisa, anaweza kumuacha mtoto ajkalia mpaka kukaukia lakini haamki, aliacha kunipiga lakini vituko vya wanawake, kila siku kupigiwa simu kutukanwa nikajikuta na mimi narudi hali ileile ya zamani, nilikua nawapiga wanangu bila kujali mdogo au mkubwa, niliacha kuwapiga wanangu pale mwanangu wa mwisho akiwa na miezi sita.


Ilikua ni usiku, mume wangu alikua bado hajarudi, mtoto alikua analia sana, anataka kunyona uila maziwa hayatoki, nikimpa ya ng’ombe mtoto hataki kunywa, siku hiyo nilihisi kuchanganyikiwa kwania alivyokua analia nilimpa mpaka ugali mtoto wa miezi sita lakini hakunywa. Nilimpigia simu mume wangu ili kulete maziwa ya mtoto lakini ilipokelewa na mwanamke akaanza kunitukana, alinitukana sana.


Nakumbuka mtoto alikua begani bado analia, nilimchukua mpaka kitandani nikamlaza na kumuacha hapo, nilitoka nnje ili kupumua lakini bado alikua analia, nilirudi ndani nikachukua mto na kumfunika nao, nilitaka kumnyonga ili anyamaze. Lakini wakati nikifanya hivyo mtoto wangu mkubwa ambaye wakati huo alikua na kama miaka kumi aliingia, alinishika huku naye akinitukana akianiambia mimi ni mnuuaji nataka kumuua mdogo wake.


Mtoto wangu wa kwanza ni wakiume hivyo kutokana nakero za pela nyumbani namna nilivyokua nampiga na kuwapiga wadogo zake, pombe za Baba yake na matusi ya kila siku alsihazoea, alikua na hasira sana na mara nyingi nikiwapiga waodgo zake alikua akinitukana sana na kuniambia akipata pesa ataondoka na waogo zake na hawatarudi tena.


Nilikua namuambia aindoke na mara nyingi kumpiga tunapigana, hakua na umbo kubwa ila kwa hasira zake alikua anaweza kuokota chupa akakupiga nayo, kama ana kisu atakurushia yaani ni chochote kile. Nilijisikia vibaya laiponiita muuaji, hapo ndipo nilishtuka na kuona kuwa kweli nilikua namuua mwanangu kwasababu ya mwanaume. Niliacha kufanya nilichokua nakifanya, nikatoka nnje, mtotoa lichukuliwa na Kaka yake, akambembeleza na kunywa maziwa, hakumrudisha chumbani kwangu mpaka subuhi.


Sikuwapiga tena wanangu nilijaribu kubadilika ili kuwa Mama bora kwani pamoja na hasira juu ya mume wangu bado nilikua nawapenda sana, niliwapenda kuliko kitu kingine chochote kile, sijui kwanini nilikua nawapiga ila nilikua najua nawapenda tena sana. Nilibadilika na kuanza kuwa na upendo, lakini miezi miwili tu baadaye mtoto wangu wa kwanza alianza kuumwa, alipata kitu kama uvimbe kwenye mguu, ulianza kama masihara lakini hali ilizidi kuwa mbaya, akafikia hawezi kabisakutembea.


Alikua anachoka, halali maumivu yalikua makali sana. Baada ya kwenda hospiitalini ndipo tuliambiwa kuwa mtoto wetu ana Kansa ya Mguu. Ilikua ni habari mbaya sana kwetu, mume wangu aliposikia alichanganyikiwa, kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu mume wangu alikua Baba kwa watoto wake, aliacha pombe, tukaanza kuhangaikia matibabu, haikua katika hatua mbaya tuliambiwa kabisa kuwa anaweza kupona lakini kusikia tu naneo kansa iliumiza sana.


Kwa mtoto yeye hakuonekana kuogopa kuhusu kuugua, sijui alijulia wapi lakini ni kama alijua kuwa anakufa, alijua kuwa hawezi kupona, wasiwasi wake mkubwa ilikua ni waodgo zake. Wanangu walikua wanampenda sana Kaka yao, yaani hata yule mdogo kabisa wote walikua wanampenda, alikua anawaambia namna ya kuishi, hawaambii kama atakufa lakini kila sikua likua anawahusia.


Mtoto wangu wapili alikua na miaka sita kuingia saba, wakike lakinia kili zake zilishakomaa. Alikua akimsikiliza Kaka yake, akienda hospitalini basi wataongea sana anawapa wosia. Bada ya matibabu na kukaa hospitalini kama miezi miwili hivia liruhusiwa kutoka hospitalini, hali yake ilikua nzuri kidogo lakini hali ilizidi kuwa  mbaya na ilionekana anatakiwa kukatw amguu, baada ya kuambiwa wala hakuonekana kuumia alisema yeye ni sawa tu.


“Mama siwezi kupona hivyo hata nikikatwa kichwa sitajali, siuhitaji huu mwili ila nina waiswasi na wadogo zangu.” Nakumbuka maneno yake aliyoniambia, hakuonekana kujali kuhusu yeye ila alionekana kukata tamaa kabisa. Nilijaribu kumpa moyo lakini hakuonekana kama ana hamu ya kuishi, kila wakati alikua ananiambia atakufa na alitamani aondoke na waogo zaake kwani akiwaacha watateseka.


Niliona kama ni hasira tu na kukata tamaa mpaka siku moja kabla ya sisi kumrudisha Hospitalini aliniomba sana kubaki na wadogo zake chumbani, ni kama alikua anwaaga. Ingawa nilikua bado sijakata tamaa lakini nilimruhusu kwani kwa namna alivyokua anaumwa hata mimi nilikua na wasiwasi, nilikua sina imani sana kama atapona.


Niliwaingiza chumbani wadogo zake wote, mara nilimuona wanangu wakike akitoka na kuchukau jagi la maji, aliniambia Kaka yake ana kiu. Lakini walikaa huko ndani kimya kama lisaa lizima bila kutoka, sikusikia kelele za mwanangu mdogo kulia ambaye wakati huo alikua anakabia mwaka wala watu kuongea, mume wangu ambaye tangu mtoto kuanza kuumwa muda mwingi aliuutumia nyumbani alikua ndiyo anarudi.


Aliniuliza watoto wako wapi nikamuambia wapo ndani Kaka yao ni kama anataka kuwaaga, lakini sijui ni nini kilimpata mume wangu bila hata kunijibu alikimbilia mpaka ndani, mlango ulikua umefungwa kwa ndani kitu ambacho hakikua cha kawaida, aligonga mlango lakini haukufunga, aliupiga teke haukufunjikaa akachukua jiwe na kuupiga, akafanikiwa kuuvunja mlango.


Watoto wetu wote watano walikua wamelala kitandani mapovu yanawatoka. Tuliwafuata na kuanza kuangalia, wawili yule wa kika wa pili na watatu walikua hawapumui kabisa, tayari walishafariki dunia. Mtoto mdogo yeye alikua kama kalala, alikua na mapovu ila bado alikua na pumzi. Mtoto wa nne naye alikua na pumzi kwa mbali na mtoto wa kwanza alikua anapumua kwa shida sana.


Nilikiambia kuita majirani, katika kuwawahisha hospitalini mtoto wa nne naye alifariki dunia. Wakabaki wawili, mdogo yeye alipata nafuu siku ileile ila mtoto wangu wa kwanza aliendelea kubaki hospitalini akipumulia mashine. Nyumbani kule ndipo tuliona kakaratasi.


“Nilikua na miapngo mingi kuhusu wadogo zangunikimaliza shule niwachukue niondoke nikakae nao lakini sitaweza, nitakufa hivi karibuni najua hamtupendi hivyo siwezi kuwaacha wadogo zangu kuteseka na nyie, Baba, Mama tumeamua kuondoka tukapumzike.”


Wanangu wawili walishauriana nini kitatokea, wakaamua kukoroga sumu ya panya wakawanywesha wadogo zao na wao kunywa ili tu Kaka yao akifa asiwaache waondoke wote. Ulikua ni mkasa wa ajabu, maisha ni kama yalisimama, nilitamani kumlaumu mume wangu lakini haikuwezekana, nilijilaumu sana kwani nilijua kwa kiasi kikubwa mimi pia nilichangia.


Mtoto mkubwa alitoka hospitalini kwasababu ya sumu lakini alikatwa mguu na kupona kabisa ila hakua sawa tena. Tangu kugundua kuwa wadogo zake watatu wamekufa nayeye kabaki peke yake na mdogo wake wa mwisho maisha hayakua sawa kabisa, alipona kidonda lakini hakupona akili, alikua kama mtu aliyechanganyikiwa, amenyamaza tu.


Tangu kitendo kile kutokea mpaka leo hajwahi kunyanyua mdomo wake hata kuita neno Mama, tumehangaika neye kila sahemu lakini ni kama amechanganyikiwa, anaweza kusimama wima sehemu hata masaa mawili mpaka umshike au kumlazimisha kukaa, anaweza kukaa masaa mawili anaangalia ukuta huku machozi yakimtoka bila kuongea chochote.


Ingawa mimi na mume wangu tunajitahidi sana kuwa kama familia tena lakini hatuna amani, tunaishi tu na kujilazimisha kucheka kwaajili ya watoto ila maumivu ni makubwa. Kila nikikumbuka mambo mume wangu aliyokua akinifanyia na mambo ambayo nilikua mnawafanyia wanangu natamani hata na mimi kufa lakini nikiwaangalia wananguwa liobaki najua kabisa wananihitaji. Maisha yemakua magumu sana, najaribu sana kuilazimishia furaha lakini bado siioni, sioni mwanga kabisa.

MWISHO

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top