MANARA AKUBALI KUOMBA YAPITE ALIYOYASHTUMU,KAZI KWA SIMBA SC KUAMUA KUMTOA AU LA!.

0

Bila shaka ungependa kujua hatima ya Manara msemaji wa Club ya Simba Sc baada ya Tuhuma alizozitoa kupitia mtandao wa Instagram,wakati huo katika mitandao mingine zikisambaa sauti za kumlaumu CEO wa Club hiyo Barbara.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Haji Manara ameandika andiko lingine ambalo unaweza kusema kama mambo yamekaa sawa kwenye mvutano huo au unaweza sema yeye ameamua kuachilia lipite sasa kusubili hatima ya waajiri wake ikiwa atasamehewa au la!.

Hili ndio andiko lake kupitia Instagram.

Kuanzia Siku ya Jumatano hadi leo ndizo siku nilizoongea na simu nyingi zaidi na kwa muda mrefu pengine kuliko Siku zote za maisha yangu.. 

Lakini WhatsApp na DM ndio ilikuwa balaa, hapo usiniulize SMS na E-mail. 


Yes kila mmoja akiniambia lake , kiukweli nimewasikia na kama Binadaam acha tungoje asili ichukue nafasi yake. 


Mwenyekiti wa Simba HQ Farouk Baghoza TSN , Mbunge na Mwanachama wetu maarufu Mh @jmakamba , Makamu Mwenyekiti wa Bodi Salim Try Again , ambao tumefanya conference calls nyingi na wote wengine nimewaelewa. 


Sitaongea lolote Kwa sasa nikiamini katika maslahi makubwa ya Simba, team ya maisha yangu. 


Captain wangu @john_22_bocco always naamini ktk ww linapokuja Nahodha wa mfano, tuliongea nikiwa ktk bad mood lakini nasaha zako na Kwa heshma ya jana ninakataaje Kwa mfano kukusikiliza?


Washabiki wote wa Simba na Waandishi mliokuwa na hamu na press yangu Am Sorry , acheni Ibilisi aepukwe ngoja tusubiri mchanga wa Pwani. 


Kimsingi nimemaliza sina lingine ila walioumia Kwa ajili ya Simba ,again poleni na Samahani.


Kwa wale akina sie niwaambie ndoo ya maji haijazwi upepo 


Af'wan 🙏


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top