Jeshi la polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu watatu kwa mahojiano wakidaiwa kulichoma moto gari la ofisa mtendaji kata ya Ilagala, .
Akizungumza leo Jumanne Julai 6, 2021 Kamanda wa polisi mkoani humo, James Manyama amesema tukio hilo limetokea Julai 4, 2021 eneo la Kugongoni A kata ya Ilagala wilayani Uvinza.
Huku akieleza kuwa gari ni aina ya Toyota Probox amesema, “watu hawa waliingia lilipoegeshwa gari na kufunga utambi walioulowanisha na petroli. Thamani ya gari hilo ni Sh13.5 milioni.
Mpaka sasa tunawashikilia watu watatu kwa mahojiano na uchunguzi ukikamilika sheria itachukua mkondo wake.”
SOMA HII Je! unajua Tabia yako inatokana na kundi la damu yako?