MBOWE: UTOAJI WA CHANJO YA #COVID19 TANZANIA UWE WA LAZIMA

0


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameomba huduma ya utoaji Chanjo ya Corona iwe ya lazima badala ya hiari kama ilivyotangazwa na Serikali.

Mbowe amesema “Serikali inasema Chanjo ya COVID-19 ni hiari ya Mtu, akatayependa ndiye apewe. Huu sio utaratibu wa WHO. Kwa wenzetu chanjo ni lazima, tunamuomba Mama Samia aweke utaratibu wa chanjo kuwa lazima na inapaswa itolewe kwa kila Mtu, huu ugonjwa unaua”

Akiongea kuhusu gharama za Matibabu amesema ”Mgonjwa wa #COVID19 ukilazwa ni zaidi ya Tsh. milioni 10 kwa wiki 2. Nimeuguza Ndugu yangu Moshi, kwa siku anatumia mitungi minne kila mtungi elfu 30, ni Watanzania wangapi wanamudu? Gharama zinapaswa kubebwa na Serikali sababu WHO imetangaza ni Janga la Taifa.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top