"Nimesoma na kupokea maoni,ushauri na kila aina ya hisia ambazo naamini ni kwa upendo juu ya Clip yangu kuhusu kambi za Kitaaluma nilipokuwa nikizungumza na wananchi wetu katika tafsiri yoyote ile naomba Radhi kwa wote waliokwazika ,wananchi na Viongozi wenzangu hasa pale matumizi ya neno "Waziri" lilipobeba hisia tofauti nawaheshimu Mawaziri wote na nafanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa natambua pia kazi nzuri inayofanywa na Mawaziri wetu wanaosimamia sekta ya elimu - Wapo wanaodhani maelezo ya hisia zangu ni kuanza kupandisha mabega,na pengine mgema akisifiwa tembo hutia maji-niwaondoe hofu sina sababu ya kupandisha mabega." AMEANDIKA RC WA DODOMA, ANTHONY MTAKA KUPITIA UKURASA WAKE WA Instagram @Antonmtaka
Itakumbukwa Jana katika mitandao ya YouTube ilikuwa imepakia vidio ya Mkuu Hugo mkoa akionekana kukosoa kauli ya mawaziri juu ya elimu kuchangia michango na kuweka kambi za wanafunzi ili kuchangia ufaulu.