Polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Makindu, katika kaunti ya Makueni wanamzuilia mvulana mwenye umri wa miaka 16, kwa shutuma ya kumuua bibi yake mnamo Jumamosi, Julai 24 usiku
Mshukiwa huyo anaripotiwa kumuua Milcah Mwendo mwenye umri wa miaka 67, katika kijiji cha Usungu eneo la Kiboko. Gazeti la Taifa Leo Jumatatu, Julai 26, linaripoti kuwa mwili wa Milcah ulipatoka na mumewe Joseph Mungutu Nthungu mwendo wa saa nane adhuhuri. Akiri kuua Kulingana na ripoti ya polisi, mshukiwa aliyetambuliwa kwa jina Stephen Mungutu Mutua, alikiri kuingia nyumbani kwa marehemu na kumnyonga akitumia kitambaa cha meza