MWANAMKE WA KWANZA KUWANIA URAIS TANZANIA AFARIKI DUNIA.

0

 


Mwanamke wa kwanza kuwania urais nchini Tanzania Anna Elisha Mgwhira amefariki dunia leo julai, 22,2021 akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru Jijini Arusha Kaskazini mwa nchi, maradhi ambayo hayajawekwa bayana mara moja.


Mwanamama huyo alijitupa ulingoni mwaka 2015 kupitia chama cha ACT Wazalendo, kuuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uchaguzi ambao ulikuwa na ushindani mkubwa kati  ya waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasa na Rais wa zamani wa Tanzania John Magufuli ambaye alishinda kwa kupata asilimia 58.46 ya kura zote.


Mghwira alikuwa Mgombea pekee aliyehudhuria shughuli ya Mshindi wa uchaguzi huo John Magufuli kukabidhiwa cheti cha ushindi katika uchaguzi huo, hatua iliyomfanya kuwa mpinzani wa kwanza kuteuliwa kuhudumu kwenye serikali yake.


Mzawa huyo Januari 23, 1959 Mkoani Singida amefariki Dunia miezi michache baada ya kuondoshwa kuhudumu wadhifa wa Ukuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alioanza kuhudumu tangu mwaka 2017 alipokihama chama cha ACT Wazalendo na kujiunga na Chama tawala cha mapinduzi CCM.


Familia ya mwanamama huyo nguli wa masuala ya sheria imeliambia Gazeti la mwananchi kuwa alizidiwa kabla ya kuingizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.


"Ni kweli Mghwira amefariki mchana huu, alikuwa amezidiwa akawa amepelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)," amesema mdogo wake.


Zaidi ya wiki moja iliyopita alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua ambapo baadaye hali yake kuwa mbaya alihamishiwa hospitali ya Mount Meru.

Soma zaidi>> WASIFU WA ANNA MGWIRA

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top