BINTI; Kaka najihisi tu kuchanganyikiwa, nina miaka 25, ndiyo nimemaliza chuo na nina kazi yangu. Kaka mimi ni mwembamba sana kiasi kwamba nahisi hakuna mwanaume wakinipenda, Kaka nimekua mpweke, sitongozwi yaani naona kama wanaume wananikwepa, nina mawazo sana Kaka kuna wakati natamani hata kujiua kwani nikiona wenzangu wanatongozwa basi naona kama mimi nitakufa peke yangu, nisaidie nifanye nini Kaka.
Kuna Kaka mmoja aliwahi kunitongoza, baaada ya kutembea na mimi nikagundua kuwa kumbe alikua kabet na rafiki yake kuwa anaweza kunipata ndani ya siku moja. Wakati niko naye chumbani akampigia simu rafiki yake akaja kuona, kaka niliumia sana, nilikunywa vidonge lakini ni Mungu tu nikaokolewa na mpaka sasa sijawahi kutamani kuwa na mwanaume tena.
Kuna watu wananitongoza lakini kila nikitaka kumkubalia basi naona kama vile naye atanidanganya, naomba nisaidie nifanye nini kwani nimekata tamaa kabisa sitamani kuishi.
IDDI MAKENGO; Umeenda hotelini kununua chakula, unaagiza chakula kabla ya kula mhudumu anaanza kulalamika kuwa hiki chakula ni kichafu, kimeoza na sikudhani kama kuna mtu angekila ila nashukuru wewe umekiona, je utaendelea kula au utaacha?
BINTI; Nitaacha Kaka?
IDDI MAKENGO; Kwanini uache wakati bado hujakionja, labda ungekionja ungekuta ni kitamu na mhudumu alikua anadanganya?
BINTI; Hapana Kaka, nisingeonja, yaani mhudumu ambaye labda ndiyo mpishi ananiambia kuwa ni kibaya halafu mimi nile, hapana, nisingegusa hata kama ningekua nimelipia basi ningekiacha na asiponirudishia pesa namuachia.
SIKILIZA SIMULIZI AUDIO
''PENZI MASLAHI"
IDDI MAKENGO; Nadhani umeshapata jibu, hutongozwi si kwakua wewe ni mbaya bali kwakua wewe unajiona mbaya, unajichukia, unahisi una kasoro ndiyo maana kila wmanaume anakukwepa. Najua huwaambii lakini kuna wakati anaweza kuja mtu, akakutongoza lakini ukajihisi kama anakutania, ukawa unamzungusha zungusha, au kwakua unajiona mbaya ukapaniki hata kuongea naye ukaona shida.
Mdogo wangu kila mwanaume ana aina yake ya wanawake ambao anapenda kwamba kila mwanaume anamwanamke wake, mfano, nina rafiki yangu hatembei na mwanamke mfupi, yaani akiona hata hageuki, lakini mimi nikiona mwanamke mfupi nachanganyikiwa, yaani nimuangelie kwa chini kuleee, yeye ananishangaa na mimi namshangaa ndiyo maisha.
Nina rafiki yangu mwingine yeye anapenda mwanamke aliyejaa, mnene na kifua kiwe kimejaa haswaa, mwingine anapenda wembamba, ndiyo maisha. Kama utachukulia wembamba wako ni ugonjwa au laana kila mtu atakuona una laana ni mbaya, kama utauchukia ufupi wako, urefu, unene, weusi, weupe basi kila mtu atakuona hivyo hivyo, anza kujipenda, acha kutangaza upweke.
Hakuna mtu mbaya kwa kila mtu bali kuna mtu mbaya kwa mtu flani. Huhitaji kupendwa na wanaume 100 bali unatakiwa kutafuta 1 tu ambaye hupenda wembamba. Anza kujipenda, jikubali, baada ya kuona wembamba wako kama ugonjwa basi ona kama umodel. Najua kuna mtu alishawahi kukutongoza lakini ukahisi kuwa anakutania, anakuchora, dada ni kawaida, kila mtu anahisi hivyo ila acha kuwaza sana.
KUHUSU HUYO KAKA; Hakuna mwanaume mwenye akili anayejiamini ambaye anaweza kufanya hivyo. Huyo ni mgonjwa na badala ya kuumizwa na alichokifanya mchukulie kama mjinga, amua kuwa na furaha, hakuna kisasi kizuri katika maisha kama kufanikiwa, nina uhakika, mwanaume kama huyo kuna kitu ambacho hajiamini, ukiangalia wengi hata hilo tendo la ndoa hajui kufanya.
Mwingine naye alishawahi kunyanyaswa kingono huko nyuma, kwa mfano, kuna dada alikuja kuniomba ushauri kuhusu mume wake, namna alivyokua anapenda kumdhalilisha, nilimuambia huyo mwanaune ana shida katika familia yake achunguze. Kuja kuchunguza kumbe mume wake alikua akiingiliwa kinyume na maumbile na Baba yake mzazi tangu akiwa mdogo.
Dada umwembamba, wewe ni model, unaweza kuamua kujiona kama mwembamba mzuri au kujiona kama kituko, ni wewe, ni macho yako! Usiruhusu maneno ya washenzi wa chache kuharibu maisha yako. Hakuna mtu ambaye yuko sawa anaweza kukufanyia hivyo, wengi ni wagonjwa hivyo wachukulie poa na fanikiwa.
MREJESHO; Najua kinaweza kisiwe kitu kikubwa kwako au kwa wengine ila naomba nikuandikie Kaka. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nipo kwenye mahusiano na nina furaha. Sijui yatafika wapi na sijali hilo kwa sasa ila Kaka hamna raha kama kuamini kuwa na wewe kuna mtu anaweza kukutamanani.
Nilikuja kwako na kukuambia kuwa mimi ni mwembamba sana hivyo naona kama watu hawatanipenda. Lakini ulinishangaa, ukaniambia vitu vingi sana huwezi amini Kaka nilianza kujiamini, nikaanza kujipenda na kuacha kujinenea mambo mabaya. Huyu Kaka alikua ni kama rafiki mtu tuliyeozeana naye sikuwahi kuhisi hata ananitamani ila nashikuru sana Kaka.
Nimejiamini, sijichukii na niliacha kuwa mtu wa kulalamika lalamika. Nilikua naona aibu hata kupost picha yangu kwenye mitandao ingawa nilitamani sana, lakini nimeanza kufanya hivyo na sijali watu wanaonaje. Kuhusu ile ishu ya yule Kaka nimeamua kumuona kama mgonjwa, nimeamua kuwa na furaha na kusahau yaliyopita, nashukuru sana.
MWISHO