NATAMANI NIFE LAKINI BADO SIJAITWA BABA~~~SEHEMU YA TATU

0


Nilimkimbilia na kumshika, alikua kajichoma kisu kweli, ingawa hakikuingia sana lakini damu zilikua zinamtoka. Kisu alishakiachia kilikua chini!

“Nataka kufa, huwezi kuwa na mwanamke mwingine, mimi ndiyo wmanamke wako, mwnamke wa maisha yako, kwanini uniache?” Aliongea huku akipiga kelele za maumivu. Nilimnyanyua na kumuingiza kwenye gari nikampeleka hospitalini, halikua jereha kubwa sana alishonwa na kuruhusiwa. Nilitaka kumpeleka kwake lakini aligoma.


     SOMA sehemu ya 1&2
NATAMANI NIFE LAKINI BADO SIJAITWA BABA


“Nataka kwenda kwako, siwezi kuishi bila wewe….” Aliniambia, sikua na namna kwa wakati ule nilijua kuwa kama nikimuacha peke yake anaweza kujiua kitu ambacho sikua tayari kukiona kikitokea. Nilimchukua mpaka nyumbani kwangu, kwakua ilikua ni usiku nilijua kwua Jack hawezi kuja kwangu bila taarifa hivyo nilikua sina wasiwasi kabisa. Nilitaka kumlaza sebuleni lakini aligoma huku akining’ang’ania kuwa ananitaka hawezi kulala mbali na mimi.


Kusema kweli nilikua nimekasirika lakini sijui ni nini ila kuna kakitu katika mwili wangu ni kama kalikua kanafurahia mambo aliyokua akinifanyia nilimpeleka mpaka kitandani ambapo alivua nguo zote nakulala. Nilimuangalia kwa tamaaa ila kila dakika nilikua nikikemea ili nisimguse.


Nilitoka kwenda kulala sebuleni, hakuniita wala kuniambia chochote, nilikaa kule kwa kama dakika kumi hivi nikasema hapana, ngoja nirudi chumbani kwangy. Kichwani nilikua namchukia lakini moyo ulikua hautaki kabisa.

“Aliniacha kwa dharau sana ngoja nikamuonyeshe, nilipe kisasai, natembea naye halafu kesho namuacha!” 


Nilimuambia huku nikielekea mlangoni, taa ilikua imewashwa, nilishika kitasa ili kufungua mlango lakini kabla ya kuufungua nilisikia mtu anaongea, mwanzo nilidhani kama ananiita anaongea na mimi labda kuna kitu anakihitaji lakini haikua hivyo, Salma alikua anaongea kwenye simu na mtu mwingine kabisa.


“Baby, nimekuambia nimepata ajali lakini husikii, angalia, gari haijaumia sana lakini nitahitaji pesa kidogo….’ Alikua akiongea kwa sauti ya mahaba huku akikugumia kwa maumivu. Nilifungua mlango kwa hasira, ile kuingia nilimuona akiongea Video call, alikua uchi wa mnyama huku kashikilia simu yake mkononi akimuonyesha huyo aliyekua anaongea naye maungo yake.


Nilipoingia aliniona, lakini hakushtuka kuniona, aligeuzia simu pembeni ili nisionekane kisha akaweka kidole chake mdomoni kama kwa ishara kuwa ninyamaze. Nilihisi kama kitu kiziro kimenippiga, yaani anaongea na mwanaume mwingione tena akiwa nyumbani kwangu, video call hgalafu anakuja na kuniambia kuwa ananipenda anataka kufa kwaajili yangu?


Aisee nilishindwa kuvumilai, nilikimbia hakarakaharaka na kumfuata kitandani, nilimvamia kama nataka kumpiga.

“Baby, Dada anaingia, nakata dada anaingia!” aliongea harahaharaka huki akukata simu. Baada tu ya kukata bila kujali mshono alinyanyuka na kunisukuma pembani.

|Unanionea wivu wa nini? Wewe sibado una mwamke wako umeschaachana naye? Umeachana naye? Nakuuliza umeachana naye?? Aliongea kwa hasira na kunigeuzia kibao kuwa sikua na haki yoyote ya kumkasirikia yeye kuongea na mwanaume mwingine kama bado nina mwanamke wangu.


“Mimi nakupenda, kama bado unanipenda na unataka kuwa na mimi naimbie, nitaachana na wanaume wote nilio nao kwaajili yako!” Aliongea kwa hasira huku akilia, kwa namna alivyokua anaongea ni kama alikua ananuilaumu mimi.

“Wewe ndiyo umeniharibia maisha yangu, umenifanya nimekua malaya, umenifanya nimekua mtu wa kutangatanga, nakupenda tangu zamani lakini hata hunijali.” Aliniambia nilishangaa alikua anamaanisha nini kusema nimekua sijali wakati tangu zamani mimi nilikua nampenda na nilikua tayari kwa chochote.


“Una akili kweli wewe mwanamke, wewe si ndiyo uliniacha na kwena kuishi na mwanaume mwingine!” nilimuuliza.

|hiyo ndiyo shdia yako George,m kimi sikua na mpango wa kukuacha, hnilichepuka kwakua nilikua naona kama hunijali, hunifuatilii, hunionei wivu, yaani unanipa kila kitu lakini hata siku moja hujawahi kukagua simu yangu, hivi wewe ni wmanaume wa namna gani? Mimi ni mwanamke, nahitaji kupendwa, nahitaji kufuatilia, nahangaika mwanangu anateseka na wanaume kila siku!


Hivi unadhani mimi napenda? Niliondoka na kukuacha lakini ulinitafuta, ulikuja kwetu hata kulia? Kwanini hata hukujidai kuwa unataaka kujiua? Hukua tayari kufa kwaajili yangu, ningejueaje unanipenda kama unachonipa ni machakula tu!” Aliongea kwa hasira huku akilia, sijui ni upendo au ni ujinga lakini kwa nusu saa nzima aliyokua akiongea kila kitu kilibadilika, alikua akinilalamikia mimi na mimi nilijiona kama vile ndiyo nimekosea.


“Kwahioyo bado unanipenda?” Niliuliza swali ambali liliibua mengine.

“Hilo ni swali kweli? Hivi wewe ndiyo wakinuiuliza kama nakupenda au la? Yaani nimefanya kila kitu kwaajiliyako, nimejaribu hata kufa kwaajili yako lakini bado unaona kama vile sikupendi?” alizidi kulia mpaka nikaanza tena kazi ya kumbembleza, nilianza kujisikia vibaya na kuhisi kuwa labda alikua ananipenda siku nyingi lakini mimi ndiyo nilikau sijui sijamuonyesha upendo.”


Tulikumbatiana na kulala mpaka subuhi, hatukufanya kitu chochote lakini usiku mzima nilikua na mawazo, kichwa kilikua kinachanganya mbaya sana, nilikua sina uhakika kama ananipenda au ananidanganya. Nilikua nawaza huko nyuma kutaka kujua ni wapi nilikosea, kuna vitu vingine alikuaakivilalamikia labda kuwa mimi simfuatilii, sishiki simu yake na vingine vya namna hiyo vilikua vyakwel, niliwaza mpaka kuanza kuamini kuwa mimi ndiyo nilikua tatizo.


*****

Asubuhi nilikua nawaza sana kama Salma atakubali kuondoka au ndiyo atasababisha vurugu. Nilikua namujua na siku hiyo nilipanga kukutaana na Jack, niliamka nikiwa na wasiwasi sana kwani sikutaka Jack jue kitu chochote, bado nilikua sijafanya maamuzi kuwa nimchukue nani, lakini kuamka yhali ilikua toafuati kabisa, salma alikua kashajiandaa anataka kuondoka, alionekana kama ana haraka sana.


Ingawa nilitaka aondoke harakaharaka lakini baada ya kumuona kama anataka kuondoka nilijisikia bibaya, nilihisi labda hanihitaji tena au anaenda kuonana na mwanaume mwingine.

“Una nini, mbona unataka kuondoka, umekuja kwangu jana unajifanya kunitaka sana lakini sas ahivi unaondoka?” Nilimuuliza huku niki8simama mlangoni nikiwa kama namzuia flani.


“Baaba sikiliza, nina maisha yangu, acha kuniletea drama, nimelala kwako jana hujanigusa halafu unataka nibaki ausbuihi ili nifanye nini?” Aliongea kwa dhara, akanisukuma pembeni na kutoka zake.

“Usije kunitafuta, nitakutafuta mimi nikiwa na shida nawewe!” aliongea huku akiondoka, hakutaka hata nimsindikize aliondoka na kuniacha nimeduwaa.


Nilijisikia vibaya lakini sikua na namna, sikua vizuri kabisa, nilikua na hasira na sikutaka kuonanana na mtu yoyote. Nilichukua simu yangu na kumpigia Jack.

“Usdije nyumbani, nina safari…” nilimuambia kwa mkato lakini hakutaka kusikia.

“Una nini mbona hukuniambia mapema?” aliniuliza kistaarabu sana, kwa namna nilivyokua naongea alishrtukia kitu, alitaka kujua sababu za mimi kuahirisha, aliniuliza kama niko sawa au naume, alikua anauliza kwa upendo sana kama mwanamek anayemjali mume wake lakini bila sababu nilijikuta namkasirikia.

“Unataka kunipanda kichwani? Hiovi una akili kweli wewe? Mbona kama hukusoma, yaani nakuambia kitu unahnibishia, unaniona mimi nani! Uhuniheshimu wewe, au kuja kwenu ndiyo imekua shida, hicho kimimba ndiyo kinakupa kiburi, sijakuoa bado ushaanza kunipangi amaisha nikikuoa itakuaje….”


Niliongea maneno mengi ya kashfa ambayo hayakua na msingi, kila nilivyokua nikizidi kuongea ndivyo alikua anzidi kuniombgha msmaaha na kwangu hasira ndiyo zilikua zinazidi kuongezeka, nilikua nakasirika sana, nilijikuta namtukana sana na kumkatia simu bila sababu. Alinitumia meseji nyingi kuulizia shida nini huku akiniomba msamaha, alipioga lakini sikupokea, mwisho niliona kero nikamblock kabisa.


Nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa, mchana nilijaribu kumtafuta Salma lakini hakupokea simku yangu. Nilipiga simu sana lakini hakupokea, kichwa kilikua hakifanyi kazi nikiwaza kama ananipenda kwanini hataki kupokea hata simu zangu. Wakati huohuo Jack naye alikua akinitafuta lakini hata nilikua sijali, jioni Jack alikuja wkangu, nilikua tu nyumbani nimejikalia sina hili wala lile.


“Una matatizo gani, upo sawa kweli?” Aliniuliza baada ya kuingia ndani, sikutaka hata aingie ndani lakini kwa namna alivyokuja nilijisikia vibaya, alikuja kistaarabu kama vile4 hakuna kitu kilichoitokea, kama vile sikumtukana kiasi kwamba nikajikuta naywea mweneywe.

“Hauko sawa,una umwa au una matatikzo gani?” Aliniuliza hukua kinisogelea kama Mama anayetaka kubembeleza mtoto ili amuembie ana shida gani.


“Sina matatizo sitaki tu kuongea kwani ulikua na shida gani, si nimekublock wewe?” Nilimuuliza kwa hasira huku nikinyanyuka, nilitaka kumkwepa lakini yeye hakujali, alikua mkimya, katulia yaani kama mtu aliyeenda hospitalini kumsalimia mgonjw awa kichaa ambaye analeta fujo.


“Naomba uondoke, mimi sitaki kuongea na wewe, naomba uondoke!” Nilimuambia huku nikimnyanyua na kutaka kumuondoa pale, lakini yeye hakujali, alitaka kukaa na kujua tatizo ni nini?

“Umenituakana kwasababu ya huyu?” Aliniambia huku akinionyesha picha kwenye simu yake, zilikua ni picha za Salama akiwa uchi kitandani.

“Umezipata wapi? Nakuuliza umezipata wapi kwanini unafuatilia maisha yangu?” Nilimuuliza kwa hasira huku nikimshika kutaka kumnyang’anya simu. Hata hakupanikii, alinipa simu ili niangalie.

“Najua jana alikua hapa kwani alinitumia hizi picha nyie mkiwa chumbani na video mkiombana misamaha, najua kila kitu lakini bado sijakasirika, nakuuliza wewe huyu ndiyo mwanamke anayekufanya kunitelekeza mimi?”


Kusema kweli sikua na majibu, zilikua ni picha za kudhalilisha, Salma akiwa kitandani kwangu.

“Angalia vizuri hizo picha maana naona kama unataka kiufuta kwa hasira, huyo mshenzi wako alikua ananitumia picha ili kuniumiza roho lakini angalaia lichofanyam, kanitumia na mafaili mengine ambayo hayanihusu. Huyu si ulisema ni mpenzi wako, mbona sasa anatembea na rafiki yako mpaka wanapiga mapicha ya kijinga!”


Aliniambia hukua kiichukua ile simu na kunionyesha picha nyingine. Niliziangalia nilihisi kuchanganyikiwa, katika kumtumia picha Jack salama alijichanganya, alimtumia pamoja na picha nyingine za wanaume wawili, mmoja alikua ni rafiki yangu mkubwa mtu ambaye alikua akinisaidia katika mambo mengi na mwingine ambaye Jack hakumjua alikua nis hemeji yangu. Ndiyo Salma alikua akitembea na mume wa Dada yangu mkubwa tumbo moja na walipuga picha.


Nilijikuta nakaa chini nguvu zimeniishia, nilishindwa niongee nini, mwili ulikua unatetemeaka kama vile nimemwagiwa maji ya barafu. Kila kitu kilikua ni kama kiini macho, nilikua najua kuwa Salama ni malaya na pengine labda hawezi kubadilika ndivyoa  livyo lakini sikudhani kama anweza kutembea na watu wangu wakaribu namna ile. Watu waliokua karibu yangu kipindi nimechanganyikiwa.


Nikiwa chizi nilikua nakaa kwa Dada yangu, mume wake ananihudumia kama mdogo wake, ananipa ushauri, rafiki yangu huyo ndiyoa likua mtu wangu wa karibu, mtu ambaye nampigai simu na kumuambia matatizo yangu, kumuambia maumivu yangu, yaani nilishindwa kujua nifanye nini.


“Unajua ni kwanini sijakasirika kihivyo? Jack aliniuliza, nilimuangalia bila kummaliza, sikumjibu chiochote lakini aliendelea.

“Wewe ni kama mtumwa kwa yule mwanamke, umemuacha akakukalia kichwani, najua hujatemeba naye kwania livyokua mshenzi angenitumia video mkiwa kitandani, huyo mwanamke ni shetani, nilifuatilia mambo aliyokufanyia nimejua ukweli wote na nataka kukusaidia….” Aliniambia, lakini kabla hata hajamaliz akuongea mlango ulifunguliwa.


Tulikua tumekaa sebuleni tukiangalianaa, Salma aliingia ni kama alikua anamfuatilia Jack na alijua kuwa atakua pale. Bila kuongea chochote alimvamia na kumpiga teke la tumboni.

“Unajifanya kuingilia ndoa za wtau basi nitakuonyesha malaya mkubwa wewe! Jack alikua hajajiandaa, kila kitu kilikua ni ghafla, aliviringika pembenai na Salma akamfuata hukohuko hukua kimpiga tumboni.


Nilijua anachotaka, alitaka kumpiga tumboni kwakua alikua anajua ni mjamzito labda ili mimba itoke. Nikasema hapana, hawezi kuniulia mktoto wangu, nilimshika na kumnyanyaua, Jack naye alisimama, wakataka kuanza kupigana lakini niliwaamua hivyo wakatengana. Salama alikua na hasira kana kwamba yeye ndiyo kaibiwa mume huku Jack akiwa katulia tu.


“Sitaki kumuona huyu Malaya nyumbani kwako, nataka aondoke, ni uamuzi wako, ni mimi au yeye?” Salama aliniambia kwa kiburi, nilinyamaza bila kumjibu, alipoona kuwa sisemi chochote alinifuata na kunikumbatia kwa nguvu.

“Nakupenda lakini siwezi kuchanganywa na huyu masikini mba mchafu, kama huwezi kumuacha basi mimi nakuacha!” aliniambia huku akiniacha na kutaka kutokan nnje.

“Nikitoka humu ndani jua kuwa sitarudi tena, nakuambia siraudi n ahata kwenye mazishi yangu sitaki uje…” aliniambia hukua kifungua mlango kutaka kutoka. Lakini sijui ni kitu gani kilinishika nikajikuta namuita.

“Subiri kwanza Salma, subiri usiondoke kwanza…” nilimuambia huku nikimkimbilia, yeye alikua kama hataki akafunga mlango kwa nguvu lakini abdo nilimfuata, jack alikua kabaki ameduwaa anaangalia tu hajui chakufanya.


Mambo ndiyo kwanza yanaanza, unadhani George anataka kumuambia nini? Je, atamrudia au itakuaje? Vipi Jack, vipi na mtoto?” Nisikuchoshe.


ITAENDELEA…..Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top