NATAMANI NIFE LAKINI BADO SIJAITWA BABA~~~SEHEMU YA NNE

0


Kusema kweli nilikua bado nampenda lakini kuna kitu kilinimbia, “Acha kua fala huyo mwanamke hawezi kuwa wako, huu ndiyo wakati wako wa kulipa kisasi.”

Salma aligeuka kama hataki vile, kwa akili yake alidhani kuwa naenda kumuomba msamaha lakini haikua hivyo. Nilikua sihitaji kabisa kumuomba msamaha, nilishaamua kuwa na furaha yangu na niliamini Jack ndiyo mwanamke sahihi wa kunipa furaha.

KAMA HUJASOMA SEHEMU 1-3 ZILIZOTANGULIA BOFYA HAPA!

 👇👯👇👯

<<NATAMANI NIFE LAKINI BADO SIJAITWA BABA~~~SEHEMU YA 1-3>>


“Umesema unaondoka hutarudi tena, una uhakika?” Nilimuuliza huku nikimshika bega.

“Ndiyo, sikutaki, umenitesa sana, huwezi kupata mwanamke mvumilivu kama mimi nakuambia, tutaona, utakuja kunitafuta!” Aliniambia hukua kiutoa mkono wangu begani kwake, alijua nishaingia laini sina cha kufanya juu yake.


“Hahhahahahah! Hhahahahahah!” Nilicheka kwa dharau,  “Sitapata mwanamke kama wewe? Hivi unafikiri kuna mwanaume mwenye akili timamu atamuomba Mungu kuwa na mwanamke kama wewe? Nakuambia hivi sikutaki, sikutaki, sikutaki! Yaani sio tu hata ukifa nisije kwenye mazishi yako! Nakuambia hivii, hata ukifa nikisikia taarifa yako kwenye Radio naivunja na hiyo Radio mbwa wewe! Ondoka mshenzi mkubwa wewe, umeona nina amani ndiyo unajifanya kujirudi nenda kaendelee kufanya umalaya wako huko! Kama nikijuia huna haja ya kujichoma kisu, niambie nitakugonga na Gari mimi mwenyewe ukafilie mbali!” Nilimuambia huku nikimtukana, nilimtukana sana tena mambo ya kuhdalilisha mpaka Jack akaingilia kati.


“Muache aondoke, si sawa unavyofanya, huyu ni mwanamke mwenzangu siwezi kuvumilia nikiona unamdhalilisha namna hiyo!” Jack aliniambia huku akimshika na kumtoa nnje. Salma alikua haamini, alijitahidi kuongea kama vile ananisuta na kuonyesha kuwa hajali chochote lakini uzalendo ulimshinda, mwisho aliishia kulia na kuondoka akiwa kanywea kama kamwagiwa maji ya baridi vile!


“Ungeniacha ningempiga, yule mwanamke hana akili kabisa, kanitesa sana sasa hivi anajifanya yeye ndiyo mnyonge, yaani anataka kunifanya mimi nijisikie vibaya! Nakupenda sana na wewe ni mwanamke wa ndoto zangu, hata siku moja siwezi kumkumbuka yule shetani, nataka nikuoe hata kesho!” Nilimuambia Jack ambaye alionekana kama vile hajafurahia, nilimuambia kuwa nataka kumuoa lakini niliona kama akili yake haiku pale.

“Una nini na wewe mbona kama na wewe unataka kuniletea kisirani chako?” Nilimuuliza kwa hasira, aliniangalia chini juu bila kunimaliza kisha akaenda kukaa bila kuongea kitu chochote.


“Unamaana gani? Mbona nakuongelesha lakini hunijibu?” Nilimuuliza huku nikimfuata, nilishaanza kuwa mshari kidogo hivyo alilazimika kunijibu.

“Sikuelewi, yaani umekua na hasira mpaka nashindwa kuelewa kama wewe ni George ninayekufahamu au ni mwingine, umeona jinsi ulivyokua unamtukana X wako, ni kama bado unampenda yaani unaonekana kama bado una hasira naye!”


“Hivi una akili kweli wewe au kichwa chako kimejaa Makamasi? Mimi ndiyo mtu wa kumpenda yule Mbwa, si umeona jinsi nilivyomtukana, yaani unataka kuniletea kisirani? Hivi wanawake huwa mnatakaga nini nyie Mbuzi!” Nilijikuta naongea kwa hsaira, niliopna kama naye ananichanganya alinyanyuka kutoka alipokua amekaa na kutoka nnje, sikumfuata mpaka alipoondoka kabisa ndipo nilianza kumpigia simu kutaka kujua ni kwanini kaondoka.


“Inamaana hujui ulichokifanya?” Hakupokea simku zangu lakini alinitumia meseji, sikuijibu lakini siku hiyo nzima nilikua nikiwaza ni wapi nilikua nimekosea sikuona kosa langu. Kwangu mimi niliona kama nilikua sawa kumchagua yeye, sikuona shida kwakua nilimtukana mwanamke mwingine nilidhani kuwa naye atafurahia lakini haikua hivyo.


Nilikaa kimya kwa siku tatu bila kumtafuta Jack nayeye hakunitafuta, nilikua na mawazo sana hivyo nilimtafuta mimi kazini na kweli alinisikiliza na kukubali kuongea. Aliniambia kuwa  siku ile alikasirika kwani ni kama nilionekana kumpenda sana Salma, kwa namna nilivyokua namtukana ni kama nilikua  naumia na nilimtumia yeye kama kumpa wivu na si kuwa nampenda.


Niligundua kosa langu nikaomba msamaha na kweli alikubali. Mahusiano yalianze tena upya lakini sasa hivi yalikua ya kasi sana, nilikua natumia muda mwingi sana kwake na mwanzo tulikua na amani ila nilishangaa kila mara tunaanza kugombana gombana bila sababu za msingi. Pamoja na kwamba nilikua nimeshaachana na Salma lakini bado nilikua naumia kuwa hajaumia vyakutosha. Nilitaka aone kuwa maisha yangu yameendelea mbele na simhitaji tena.


Tangu siku ile tulipogombana hakuwahi kunitafuta wala kuonyesha dalili kuwa ananihitaji. Nilifungua akaunti feki kwenye mitandao kumuangalia kuona kama ana maisha ya aina gani na hapo ndipo nilizidi kuchanganyikiwa. Alikua na furaha, anapost Biashara zake mtoto wake na nilichanganyikiwa zaidi siku alipo post kuwa ni mjamzito na kumshukuru Mungu. Ingawa hata mimi nilikua nikitegemea mtoto lakini niliumia kwanini nayeye anategemea mtoto?


Ni kama nilitamani asiwe na furaha tena, hali hiyo ilinifanya kuwa na wivu hivyo na mimi nikaanza kumpost Jack na mimba yake. Nilimlazimisha kupiga picha, tukaenda mpaka studio napiga picha napost kwa caption za kuonyesha kuwa tunafuraha lakini sikua na furaha.

“Anapost picha kuwa ana mimba kwakua anajua tunaenda kupata mtoto, mimi hata simuamini kama ana mimba….” Siku moja uzalendo ulinishinda, nilikua kitandani nafanya mapenzi na Jack lakini akili yangu yote ilikua kwenye picha ambayo aliipost Salma mchana wake.


Hakikua hata picha mbaya tuseme labda ni ya uchi hapa,alipost picha akiwa kashikwa tumbo na huyo mwanaume wake.

“Sema kuna wanaume wajinga, yaani anamdanganya kuwa ana mimba kumbe hana, na hata kama basi ana mimba sidhani kama ile mimba ni yake, hivi unajua kuwa anatembea na Mbunge….” Nilizidi kuongea, ni kama nilikua najiongelesha mwenyewe kwani Jack alinisukuma pembeni na kugeuka upende mwingine.


Niliongea mwenyewe kwa zaidi ya nusu saa ndipo nilishtuka kuwa nilikua nafanya mapenzi na mpenzi wangu. Alikua kajilaza kitandani kachukua mto kajifunika kichwani kama kuziba masikio ili asisikie nilichokua nikikiongea. Nilijua nimefamnya kosa hivyo nilianza kumshika tena kutaka tuendelee kufanya mapenzi.

“Sitaki bwana niache, sina hamu tena ya kufanya mapenzi na wewe usiniguse….” Aliniambia kwa hasira, hakulalamika sana, hata mimi sikua na mood ya kuendelea kufanya mapenzi hivyo nilimuacha tukalala mpaka asubuhi.


****

SIMULIZI ZA SAUTI POFYA HAPA KWENYE VIDEO.
“Leo ni maajabu unanipeleka kininiki daa Mungu mkubwa!”  Ujauzito wa Jack ulishafikisha miezi sita lakini katika kipindi chote hicho alikua akiniomba nisindikize kiliniki nilikaataa. Lakini siku hiyo mimi ndiyo nilimuambia kuwa nataka kumpeleka kiliniki, alishangaa lakini alijiandaa harakaharakakwa furaha.

“Afadhali maana wale Manesi ukienda mwenyewe wanaona kama umezaa na mizimu, hata ukiwahi utakaa kwenye foleni mpaka waliokuja na wuame zao wahudumiwe, utaona leo dakika kumi tu tusharudi.”


Aliniambia lakini mimi hata sikumsikiliza, nilikua na yangu kichwani, alishaangaa nilipompeleka kwenye Hospitali ambayo hakuizoea.

“Hapa ni wapi? Hivi unajua kuwa mimi sijagi kiliniki ya huku?” Aliniuliza baada ya kuona nimempeleka kwenye Hospitali tofauti kabisa.

“Kwani Hospitali si zilezile, utaanza kiliniki hapa kama unataka niwe nakuleta, najuana na hawa madaktari hivyo watakuhamishia huku.” Nilimuambia kwa ukali, niliona kama nataka kuleta ubishiubishi wake. Wakati tukiwa tumesimama hata kuingia hataki akiwa hajui kwanini nilimpeleka pale mara Salama aliingia, alikua na Mwanaume wake hapo ndipo Jack alijua ni kwanini nilikua nimempeleka Pale.


Bila kuongea chochote aliondoka mpaka kwanye gari, funguo nilikua nazo mimi hivyo alisimama kwa nnje. Mimi hata sikumjali, sikujali kama kakasirika wala nini, nilitaka tu Salma kupita mbele yangu ili nione kama atanisalimia au la.

“Mambo vipi?” Salma alinisalimia kwa Bashasha baada tu ya kunifikia.

“Poa habari… naona umekuja kiliniki kumbe nawewe unakuja hapa nimemleta mke wangu yule pale kaenda kusimama pale kwani hijisikii vizuri?” Nilimuuliza kwa dharau flani, huku nikijielezea mambo ambayo nilikua hata sijaulizwa, yeye hakuonekana kujali, alionekana kama yuko sawa hivyo nilizidi kukasirika na kutaka kumharibia.


“Haka kakijana ni kanani?” Niliuliza kwa dharau kabla ya kunijibu nilijifanya kujiongeza na kuzidi kuonyesha dharau.

“Ndio Bodaboda wako au maana na hali yako hiyo hutakiwi kutumia Bodaboda?” Niliuliza kwa dharau pamoja na kuliona gari lake pale. Nilikua namfahamu yule kijana kuwa ni mpenzi wake hivyo nilitaka tu kumkera.

“Huyu ni Baba wa mtoto wangu mume wangu mtarajiwa….” Alitulia kidogo huku akiniangalia kwa tabasamu kisha akamgeukia mwanaume wake.

“Baby huyu ndiyo yule Kaka nilikua nakuambia, mke wake yule pale kasimama kwenye gari….”


Aliongea kistaarabu bila kusema alichokua anamuambia kijana wake lakini nilishangaa yule kija akinipa mkono kutaka kunisalimia kiheshima. Nilikua sina namna nikaitikia tukapeana mikono kwa aibu niliondoka mpaka kwenye gari nikafungua mlango, Jack alikua bado kazubaazubaa amesimama anawaangalia, nilikua na hasira hivyo sikua na muda wa kumsubiri. Niliwasha gari kwa hasira, nikashusha kioo kisha nikaanza kumfokea.


“Unaondoka au unabaki hapa utembee?” Nilimuuliza kwa hasira, alishika mlango kuufungua nikaona kama ananichelewesha, niliachia mafuta gari ikaenda mbele kidogo.

“Harakaharaka bwana unanichelewesha wewe vipi?” Nilizidi kuongea kwa hasira, kwa namna nilivyokua nataka kuondoka kila mtu pale alishangaa kwani nilikua ni mshari shari sana. Aliingia kwenya gari harakaharaka ila hata kabla hajafunga mlango vizuri nilishaondoka kidogo adondoke na sikujali.


“Una nini mbona hivyo? Inamaana ulinielta huku ili kuja kuonana na mwanamke wako….” alianza kulalamika, mimi akili zangu zilikua kwingine kabisa, sikujali hata kama yupo mule ndani, niliendesha gari harakaharaka mpaka nyumbani, njia nzima alikua akiniongelesha kwa hasira bila mimi kujibu. Nilihisi kama anataka kunipanda kichwani, nilisikia kama ananitukana. Niliingiza gari mpaka ndani kisha nikashuka, kabla ya yeye kushuka nilienda mpaka kwenye mlango wake na kuufungua.


“Shuka! Shuka nimekuambia shuka!” nilimuambia kwa hasira, yeye bado alikua anashangaa shangaa.

“Unanilazimisha nini? Niache nitashuka mwenyewe au hata kwenye gari hutaki….”  Sikumpa hata nafasi amalizie kuongea, nilizishika nywele zake ambazo alikua kasuka rasta nikamvuta na kamrusha nnje ambapo alidondoka chini. Akiwa bado anakijizoazoa nilimshika mkono wake wa kulia na kuanza kumvuta kumuingiza ndani?


“Unataka kunipanda kichwani eee? Mimi ni mwanaume lakini naona unataka kunipanda kichwani, sasana ngoja nikufundishe heshima mshenzi wewe! Nilimuambia huku nikizidi kumvuta ndani kwa mkono mmoja, alikua akipiga kelele za maumivu huku akidai kuwa namvunja mkono wake lakini sikujali. Nilikua na hasira sana nilimvuta mpaka ndani kisha nikaingia chumbani, nilichukua pasi ambayo ilikua kwenye meza ya chumbani na kutoka nayo.


Niliishika ile pasi nikawa natumia ule waya wake kumchapia, nilimchapa sana lakini nilihisi kama vile hasikii. Niliacha kutumia mkanda wapasi nikaichukua ile pasi na kuanza kumpiga nayo kama vile mtu anaponda kitu na nyundo, nilimtwanga sana huku nikimtukana kuwa ni malaya na kumuambia hata huyo mtoto sidhani kama ni wangu.


Sijui kwanini lakini kila nilivyokua nazidi kupiga ndiyo nilikua nikisisikia raha na wakati nampiga matukio yote ambayo Salama alikua akinifanyia yalikua kichwani. Nilikua najua kabisa niliyekua nikimpiga ni Jack lakini kichwani alikua  Kajaa salama, hata nilipokua nikitukana nilikua nikikumbushia  matendo ya salma na si Jack.


Nilimpiga sana, pasi, mateke na ngumi huku nikimtukana, mwanzo alikua akipiga kelele tena sana lakini baada ya muda alitumlia kabisa, alikua haongei kitu chochote. Nilicheki mapigo yake ya moyo nakuona kama moyo umesimama. Hapo ndipo nilikua kama nimeshtuka nikajua kuwa nimeua, yaani akili zangu ndiyo zilirudi.

“Nimeua, nimeua!” Nilijikuta napiga kelele kama chizi. Wakati nikiwaza kuwa nifanye nini kwani nilishaiona jela hii hapa nilipata wazo la kumfungia chumbani. Nilimvuta mpaka chumbani kisha nikafunga mlango nikatoka. Nilitoka mpaka kwenye gari nikasema hapana, kule ataonekana na kama akikutwa humu ndani kwangu basi nitakamatwa mimi kwani hata hospitalini kuna watu waliniona.


Akili iliniambia rudi mfiche mpaka jioni ukamtupe kwani hapo chumbani si salama. Nilirudi chumbani nikamchukua mpaka choo cha ndani kulekule chumbani nikaenda nikamfungia ndani kisha nikafunga milango yote na kuondoka. Nilirudi kazini kwakua ilikua ni siku ya kazi, huko nilijifanya kama vile hakuna kitu kilichotokea.


Ili nisionekane kama mimi ndiyo nimemuua kule kazini nilianza kuuliza kila mtu kuwa amemuona Jack? Wakati natoka nyumbani nilichukua simu yake na kuizima, hivyo kila mtu akipiga alikua anaambiwa kuwa simu zake hazipatikani.

“Nilimpeleka kiliniki akaniambia nimuache nyumbani kwake atakuja kazini ila mpaka sasa hivi sijamuona na simu zake hazipatikani?” Niliomngea huku nikijifanya kuwa nina mawazo sana, sikuishia kuuliza tu watu wa kazini, hata nyumbani kwao niliwapigia kuwaulizia lengo kuonekana hata mimi nilikua simuoni.


Tayari nilishajua amekufa hivyo nilijipanga kwenda kumtupa mtaroni karibu kwake, nimwagie pombe ili kuonekana alikua kalewa na labda kupigwa na wahuni, sikutaka kuishia jela. Kusema kweli nilikua sijui kwanini nilimpiga kwani katika maisha nyangu nilikua sijawahi kumpiga mwanamke lakini kila nilipokua nampiga, kila nikinyanyua mkono nilikua nikijisikia raha nikiona kama vile uanaume wangu umerudi.


Baada ya kumpiga na kumuumiza, nikajua kuwa nimeua ndipo akili yangu ilirudi na kujiona kuwa nimefanya makosa makubwa. Jioni sikurudi moja kwa moja nyumbani, sikutaka kukaa na maiti ndani kwa muda mrefu hivyo nilikaa mpaka kwenye saa tano usiku hukubado nikipigia simu ndugu zake kumuulizia hapo na waliponiambia kuwa hawajui ndipo niliamua kwenda nyumbani ili kuchukua maiti ya Jack na kwenda kuitupa kweye mtaro karibu na kwake.


Unadhani George atafanikiwa kuitupa maiti ya Jack? Mimi sijui, muhimu kama upo twitter hembu Bonyeza hapa kuna mengi yanakuja https://twitter.com/azirani360


AITAENDELEA…

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top