NATAMANI NIFE LAKINI BADO SIJAITWA BABA—SEHEMU YA SITA

0

INAENDELEA.........

Kusoma zilizotangulia

 SEHEMU YA 1-5

Nilimsikiliza Jack na kujikuta naanza kulia kama mtoto, nilihisi mamumivu makubwa. Katika maisha yangu yote nilikua siajwahi kumpiga mwanamke, nilikua na sababu nyingi sana za kumpiga mwanamke lakini sikuwahi kufanya hivyo. Nilijua kabisa kuwa ni kitu kibaya kumpiga mwanamke, lakini siku moja tu niliamua kumpiga mwanamke ambaya hakuwahi kunifanyia kitu kibaya chochote kile.


Nilimuomba sana msamaha lakini haikusaidia kabisa, aliniangalia tu bila kusema kitu chochote, kwa masaa mawili nilikua nikilia huku nikimuomba msamaha.

“Niko tayari kukuoa, nipo tayari kuishi na wewe, nipo tayari kwa chochote kile, sitaki tena mtoto, tutaadopt mtoto, tutafanya chochote lakini usiache kazi kwani nakupenda sana na maisha yangu bila wewe sioni kama ni maisha.”


Niliongea kwa uchungu sana, yeye hakuongea kitu chochote, hakulia wala kufanya kitu chochote alikua akiniangalia tu mwisho aliniambia.

“Sihitaji kuonewa huruma, kama ni kulia nilishalia sana lakini sihitaji kuolewa kwa kuonewa huruma! Hata kama nisingetolewa kizazi lakini sihitaji mwanaume kama wewe. Nimechoka na haya maisha, sihitaji kufanya kazi, sihitaji kitu chochote, ondoka na ukawe na maisha mema.” Aliniambia, niliona kama vile ananiaga, nilihisi kama vile kuna kitu kibaya ambacho anataka kujifanyia, nilimuomba sana asije kujidhuru lakini alionekana yuko sawa kabisa.


“Hahahahahah! Hapana, siwezi kufa kwaajili yako, nataka nikuone ukiteseka, nataka nikuone ukirudia kua chizi, hicho ndiyo kisasi changu, nataka nione maisha yako yakiangamia na nakuahidi yataangamia, siwezi kufa na kukuacha ukiishi kwa amani. Ondoka nyumbani kwangu kabla sijakufanyia kitu kibaya, nilikuacha unipige kama mjinga lakini sitarudia tena hilo kosa, sina kitu cha kupoteza hivyo ondoka kwangu!”


Mwanzo aliongea kama utani, niliona kama vile hawezi kufanya kitu chochote, ila ghafla alinyanyuka kwa hasira, aliingia chumbani kwake na kutoka na Panga, nilinyanyuka harakaharaka huku nikumsihi asijekufanya kitu kibaya. Lakini kabla ya kuongea alirusha lile panga, nilinyanyua mkono kulikwepa alinikata mkono na damu zilianza kutoka.

“Kaa mbali na maisha yangu mshenzi mkubwa wewe! Yaani umenipiga kama mbwa halafu unakuja kuniomba msamaha, utarudisha kizazi changu wewe shetani? Umemgeuza Mama yangu mpaka akaniona kama nina laana, yaani umefanya mpaka naonekana mshenzi naiaibisha familia yangu halafu unakuja hapa unajifanya kujali? Hunijui wewe mbwa ondoka, sina cha kupoeza mbwa kabisa, nisikuone kabisa katika maisha yangu!”


Aliongea kwa hasira sana hukua kinifuata, nilijua kuwa alikua hatanii na alikua hana chakupoteza, alikua kama chizi hivyo nilitoka mbio na kuingia kwenye gari kisha nikaondoka. Damu nyingi zilikua zikivuja kwani alinikata pakubwa, nilivua shati na kufunga mkono lakini damu zilizidi kunitoka, sikua na namna zaidi ya kwenda hospitalini.

“Vibaka, walikua wanataka kuninyang’anya gari lakini nimefanikiwa kuwadhibiti.” Niliwaambia, nilipatiwa huduma ya kwanza, kwakua walikua wakinijua kulikua hakuna haja ya kwenda Polisi.


*****


Siku tatu sikwenda kazini, nilikua naumwa na bado kichwa changu kilikua hakijakaa sawa, nilikua na mawazo sana kuhusu Jack nikiamini kuwa kachanganyikiwa na anaweza kuharibu maisha yake kwaajili yangu. Kichwa kilikua kinauma, nilikua na mwazo sana nikiwaza kumtafuta mtu wake wa karibu ili kumuambia kuhusu Jack, hali yake iliniumiza sana kwani ni mtu ambaye hakua mbaya kwangu, lakini kila nikiwaza kuongea na ndugu zake nilikua naogopa, alishaniambia nikae mbali na familia yake hahitaji msaada wangu kabisa. Roho ilikua inaniuma lakini nilikua sina namna ya kuweza kumsaidia kabisa.


Nilienda kazini nikijua kuwa ashaacha kazi, ile nafika tu nilikutana na Afisa Utumishi ambaye aliniita pembeni.

“Sijui ni kitu gani umekifanya lakini umensaidia sana, yaani amerudi kazini na jana kapata barua ya kupandishwa cheo, amekua Mkuu wa Idara, yaani kuumwa kwake imekua kama baraka kwake.” Afisa utumishi aliniambia huku akitabasamu. Ingawa nilikua najua kabisa alikua akimzungumzia nani lakini nilikua kama nimeshikwa na bumbuwazi, nilibaki kimya nikishangaa.


Nani huyo kapandishwa cheo? Nilimuuliza kwa mshangao kama vile sijui chochote.

“Jack, ndiyo Bosi wetu sasa hivi, anaandika barua ya kuacha kazi hukua anapandishwa cheo….” Aliendelea kuongea lakini sikumsikia, ni kama alikua anaongea na mtu mwingine kabisa. Nilijisikia vibaya, nilijisikia kuchanganyikiwa yaani kila kitu kilikua tofauti kabisa, nilimuacha Afisa Utumishi kasimama, nikaingia ndani kama chizi, kila aliyeniona alijua sipo sawa.


“Unaitwa kule ndani….” Ukiingia ofisini kwetu kitu cha kwanza unakutana na sehemu ya kusaini kwa kutumia vidole, pembeni yake kuna dada wa mapokezi ambaye kazi yake ni kuwaelekeza wageni, kupokea simu zote za ofisi na kuziunganisha na wahusika na kuulizia kama mtu flani yuko tayari kuonana na mtu flani. Basi nilipoingia tu ni kama alikua ananisubitia, aliniambia niingie katika ukumbi mdogo, niliingia huku bado nikitetemeka.


Huko nilikuta wafanyakazi wenzangu wa ngazi za chini wamekaa wanasubiria. Niliingia na kukaa, kama dakika tano hivi Jack alingia akiwa kaongozana na Mkurugenzi Mkuu pamoja na wakuu wenzake wa idara, wote tulisimama kwa heshima mpaka walipokaa. Kusema kweli sikusikia kitu chochote mpaka wanatoka, tulikaa kwa zaidi ya nusu saa ila sikusikia kitu, akili yangu ilikua ikiwaza maisha yangu ya pale, ningeishije na Jack kama Bosi? Kwa cheo chake kipya hakuna kazi ningeweza kuifanya bila kuruhusiwa nayeye, hakuna pesa ningeweza kuingiza bila kupata kibali chake, nilimuangalia nakuona maisha yangu yameisha.


Walitoka na kuondoka wakati natoka tena dada yuleyule aliniambia naitwa, alinielekeza ofisi ya Jack. Niliingia na kuona amekaa ananisubiria, tofauti na nilivyodhani kuwa atakua na hasira, ataniangalia kwa dharau au kitu kingine chochote kile lakini alinikaribisha vizuri, akaniambia anaamini tutafanya kazi vizuri kwakua sasa sisi si wapenzi hivyo akanisihi kuwa mimi nayeye ni kama hatujawahi kujuana hivyo nimeheshimu kama Basi wake.


“Kama hutaweza kufanya kazi na mimi niambie, uandike barua ya kuacha kazi kwakua hakuna namna nyingine zaidi ya hiyo!” Aliniambia kwa ukali kidogo, ni kitu ambacho nilikitamani lakini sikua na namna, nilishapitia maisha ya kutokua na kazi, kuhudumiwa na ndugu, nilikua naishi kwa shemeji yangu, yaani nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa hivyo sikua tayari kabisa kwa hilo.


“Hakuna shida, mimi niko sawa nitafanya kazi nawewe vizuri na naamini kuwa hakutakua na shida. Yaliyotokea ni makosa yang…” Nilimuambia lakini hakua tayari kusikiliza alinikatisha.

“Nyamaza, hakuna kilichotokea, ulikua ni mpenzi wangu tumeachana mengine hayakuhusu, fanya kazi kama huwezi andika barua ondoka!” Aliniambia kwa hasira kidogo, nilibaki kimya bila kuongea chochote kwani nilijua sasa hivi ni Bosi wangu na kwa nafasi yake alikua na uwezo wa kunifukuza kazi wakati wowote, nilimsikiliza alivyokua anataka mwisho akaniambia nitoke kwani ana kazi nyingi za kufanya hukua kinisisitiza kuwa mimi nayeye hatujawahi kuwa wapenzi.

“Mambo ya afya yangu hayakuhusu kabisa, nikisikia nitasahau kama nilishawahi kukupenda, naamini unakumbuka kichaa changu? Hii kazi ndiyo kila kitu changu ukijaribu kuiharibu sitadili na wewe, safari hii panga litaanzia kwa Mama yako na kumalizikia kwa familia yako nzima, si unajua sina cha kupoteza!” Aliniambia huku akicheka lakini alikua akimaanisha.


****


Maisha ya pale kazini yalikua tofauti na nilivyodhani, Jack alikua Bosi wangu kweli, hakunibagua wala kunifanyia toafauti na wengine, alikua akinifanyia sawa, anaongea na mimi vizuri na safari za kikazi alikua akinipa sawa na wengine. Alikua ni Bosi mzuri na kila mtu alimpenda, kwanza aliwapa uhuru walipo chini yake wa kutimiza majukumu yao, alikua akielekeza zaidi ya kugombeza na kubwa zaidi alikua akitoa safari za kikazi kwa mzunguko.


Unapokua kazini kitu kikubwa kinachoingiza pesa zaidi ya mshaara ni safari za kikazi. Ofisi yetu ilikua na safari nyingi sana za kikazi lakini huko nyuma bosi ndiyo alikua akienda na watu wake wachache. Baada ya kuingia Jack aliweka utaratibu wa Mzunguko, aliitisha kikao na kutuambia kuwa safari zote ambazo hazimhitaji Bosi mwenyewe au mtu flani mahususi zitakua ni safari za kugawana, kutakua na zamu ya kila mmoja wetu. Kila mmoja zamu yake ikifika hata kama ni nnje ya nchini basi ni bahati yake hivyo ataenda na hataingilia.


Mwanzo hatukuamini ila baadaye ilikua ni kawaida na kila mtu alimpenda na kazi zilienda vizuri. Alikua na furaha na kulikua na tetesi kuwa yuko kwenye mahusaino na Mzungu mmoja ambaye ni rafiki yake anakuja kuja pale ofisini. Hali hiyo ilinitesa sana kwani alikua na furaha bila mimi, ingawa hakua akionyesha mahusiano yake wasiwasi lakini nilimfuatilia na kugundua kuwa ni kweli alikua kwenye mahusiano.


Nilihisi kuchanganyikiwa kwani mimi mwaka ulikua umepita bila kuingia kwenye mahusiano na mwanamke yoyote. Huku nyuma nilisikia Salma naye kaolewa, yaani nilichanganyikiwa zaidi kwani yeye alikua ni mtu wa kujionyesha, mara nyingi anapost picha kwenye mitandao namna alivyokua na furaha. Baada ya kuona hivyo nami niliamua kuingia kwenye mahusiano, niliingia kwenye mahusiano na dada mmoja ambaye alikua ni mtoto wa field ambaye alikuja pale ofisini.


Nilimuambia kuwa sijwahia kuwa kwenye mahusiano an nilimuonyesha upendo wa hali ya juu, nilimleta mpaka kwangu na akawa kama mke wangu. Lakini siku ya kwanza nataka kufanya naye mapenzi nilikua sina hisia kabisa, haikua kawaida yangu, nilimgusa kila sehemu lakini uume wangu haukuweza kusimama.

“Una shida gani Kaka mbona hivi?” Aliniulizia huku akinichezeachezea kuona kama nitashtuka lakini wapi! Akili yangu ilikua mbali sana, nilijisikia vibaya, niliona aibu na kila alivyokua anazidi kunishika ili kunishawishi nilijikuta nazidi kupandwa na hasira.


“Unanishikia nini mchawi mkubwa wewe!” Nilimuambia huku nikimsukuma, nilikua nimelala kitandani yeye akiwa juu yangu, nilimsukuma akadondoka chini. Alipiga kelele za maumivu lakini sikujali, nilinyanyuka na kuvaa nguo huko yeye akiwa bado pale chini.

“Kwani nimefanya nini mpaka unanifanyia hivi?” Aliniuliza, hapo ni kama aliupalia moto, nilimfuata na kuanza kumpiga mateke, bila kujali kama ni usiku au nini nilimpa nguo zake, nikamsukuma na kumtoa nikamfungia nnje.


Aliomba msamaha lakini sikutaka kumsikia, baada ya kuona kuwa sijali aliondoka zake. Nilijisikia vibaya sana huku nikiona kama maisha yangu yameisha, kwangu kile kitendo kilikua ni mara ya kwanza kunitokea hivyo nilihisi nina matatizo. Nilichukua simu yangu, nikaingia kwenye mitandao ya ngono, nikaanza kuangalia video za ngono ili kuona kama tatizo ni nini?


Wakati naangalia nilishangaa nasisimkwa, nilijisikia vizuri mpaka kufika kileleni. Niliona kama sina shida nikaamini kuwa yule binti ndiyo mwenye matatizo. Keshi yake nilikutana naye kazini, nikamfuata na kumuomba smamaha ana kuomba turudiane, kweli alikuja kwangu na siku hiyo nilifanikiwa kufanya naye mapenzi vizuri kabisa kwani nilikua najiamini. Lakini pamoja na kuweza kufanya naye tendo la ndoa nilijikuta nina hasira, niliona kama naye ni mwanamke hivyo si mtu mwema kwangu.


Bila yeye kunifanyia kitu chochote nilijikuta nankasirikia na kutamani kumfanyia kitu kibaya. Wakati tuko kitanda nafanya naye mapenzi, nilijifanya kukosea njia, nikafanya naye kinyume na maumbile, mwanzo alikataa lakini nilimbania chini na kumlazimishia, alipomaliza nilimpiga sana.


“Wewe si malaya tu, una tahamani gani? Umekuja kufanya field lakini unajirahisisha kiasi hicho, wewe ni malaya na hakuna kitu utanifanya?” Nilimtukana sana huku nikimpiga, kile kitendo kilinifanya kujisikia raha, nilijisikia kama mwanaume flani, yaani nilitamani niendelee kumfanyia mapenzi namna ile lakini nguvu nilikua sina hivyo niliishia kumtumkana nak umpiga. Baada ya kumaliza nilimfukuza na kumtoa nnje, nikamuambia kuwa simhitaji tena na asinitafute tena.


Aliopndoka huku akilia akiniuliza kama alikua kanikosea nini lakini mimi hata sikujali. Baada ya yeye kuondoka mimi nilitoka kwenda club, hayakua mambo yangu, tangu kupata matatizo nilishaacha pombe lakini siku hiyo nilikunywa tena sana na nilijisikia vizuri. Kesho yake niliamka vizuri na kwenda kazini, nikiamini yule binti hatanisemesha nililpofika kazini tu ni kama alikua ananisubiria.


“Kaka naomba tuongee, naomba sana unisikilize kama kuna kitu nimekukosea naomba sana.” Aliniambia huku akitaka hata kulia, kusema kweli sikutegemea hilo,. Wakati ananiomba msamaha akili yangu ilikua kwa Salma, nilikumbuka namna ambavyo alikua ananifanyia vituko lakini mimi ndiyo naishia kumuomba msamaha, nilikumbuka namna ambavyo nilimfumania na mwanaume mwingine, akaniambia hanitaki mimi ndiyo nikapiga magoti.


“Kumbe ni raha namna hii….” Nilijikuta najisema bila kujali kama binti wa watu kasikia au la. Nilimuita mpaka ofisini kwangu na kumuambia akae.

“Una shida gani? Unataka nini?” Nilimuuliza lakini alibaki kaduwaa.

“Ondoka kama huna chakuongea, nina kazi nyingi sana, nilimuambia huku nikimnyanyuakua kutaka kumtoa kwa nguvu. Sikutaka kuendelea kuongea lakini wakati nimemshika namtoa mara mlango ulifunguliwa, nikiwa bado nashangaa Jack akaingia na kunikuta nimemshika yule binti namvuta kwa nguvu.”


“Kuna nini hapa? Binti anakusumbua? Vipi anataka kukufanyia kitu kibaya?” Jack aliuliza kwa hasira kama vile anataka kunipiga.

“Unataka kumbaka binti wa watu, wewe mshenzi nini?” Aliendelea kuongea kwa hasira.

“Niache!  Niache! Niahe! Niache! Utaniua niache!” Yule binti naye alipiga kelele kuona kama nilikua nikimlazimishia kitu. Nilimuachia huku nikitetemeka kwani nilikau kama nimefumaniwa vile.


Fuatilia kwenye ukurasa wetu kwenye ukurasa huu https://twitter.com/aziranipost 


ITAENDELEA…Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top