NG'OMBE ALIYEKIMBIA MACHINJIO ASAMEHEWA KUCHINJWA

0

 


Los Angeles, Marekani (AFP). Ng'ombe ambaye hakuonekana baada ya yeye na wenzake 40 kutoroka machinjio ya jijini Los Angeles, alionekana Alhamisi ya Juni 24 lakini tofauti na watoro wengine, hatachinjwa baada ya mwandishi wa nyimbo kuingilia sakata hilo kwa niaba yake.

Ng'ombe hao walisababisha sekeseke wakati walipotoroka machinjioni Jumanne jioni (Juni 22) na kuingia mitaa ya makazi ya jiji la Los Angeles, wakizurura na kuingia katika bustani za watu.

Mashefu waliokuwa wakisaidiwa na polisi kuwafuatilia ng'ombe hao, walichukua saa kadhaa kuwadhibiti na kuwapandisha kwenye trela kwa ajili ya kuwarejesha machinjioni.

Walitoroka kutoka kiwanda cha kusindika nyama kwa kupitia lango lililokuwa wazi. Polisi walimuua mmoja kwa risasi wakati alipoonekana kuikimbiza familia moja na watoto, na hatimaye ng'ombe 38 walirejeshwa machioni kukutana na kisu.

Lakini mmoja wao hakupatikana siku hiyo hadi Alhamisi asubuhi, alipoonekana akila majani eneo lililo mbali na machinjio.

SOMA PIA HII Jifunze kutengeneza fedha kupia simu yako.
Ofisa wa manispaa ya Pico Rivera alisema ng'ombe huyo atapelekwa sehemu ya kutunzia wanyama, badala ya kumpeleka machinjioni, baada ya Diane Warren, mwandishi wa nyimbo wa California ambaye ameshinda tuzo za Grammy, Emmy na Golden Globes kutokana na ustadi wake, kuingilia kati.

Hali kadhalika mji wa Pico Rivera uko kwenye mazungumzo na mmiliki wa machinjio hayo kuhusu uwezekano wa kupeleka ng'ombe wanaotoroka katika eneo la kuwatunzia, ofisa huyo alisema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top