Watoto wawili wakike na wakiume (mapacha) wenye umri wa Miaka 9 na wakiume mmoja mwenye umri wa Miaka 11 watekelekezwa na Baba yao mzazi katika Nyumba wanamoishi na baba huyo aliyefahamika kwa Jina la Edward Chaula kuondoka na kuikataza jamii kuto kutoa msaada wowote kwa watoto hao.
Tukio hilo limebainishwa July 27,2021 na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpechi Kata ya Mjimwema Mjini #Njombe Onesmo Kilasi wakati wa mahojiano yake na Kings Fm baada ya kupata taarifa za tukio kutoka kwa rai wema.
Amesema jamii ilibaini kuwa watoto hao wametelekezwa baadaya watoto hao kuonekana wakizagaa mitaani wakiiba kuku ili wafanye kitoweo na kuacha kuhudhuria Shuleni ndipo Balozi Msaidizi wa Mtaa huo aliwachukua kuwafikisha Ofisi ya Mtendaji ili kupata kibali cha kuwapelekea Wilayani Ludewa aliko Mama wa watoto hao.
Chanzo cha utelekezaji wa watoto hao inatajwa kuwa ni migogoro iliyopo kati ya wazazi wao ambapo baba anatajwa kuwa amekuwa akimtishia usalama mama yao ajulikanaye kwa jina la Andowise Mtega endapo atafika maeneo ambayo wanaishi watoto hao.