PENZI LA Grand P LAVUNJIKA RASMI.SABUBU NI HII.

0

 


MWIMBAJI na mwanamitindo maarufu nchini Ivory Coast, Eudoxie yao ameanika kuwa penzi lake na msanii maarufu wa Guinea, Moussa Sandiana Kaba Grand P limevunjika rasmi.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Eudoxie amesema kuwa ameshindwa kumvumilia Grand P kutokana na tabia yake ya kuchepuka na wanawake wengine hali ambayo imekuwa ikimnyima raha yao na sasa kuamua kuachana naye jamaa huyo anayedaiwa kuwa na mkwanja wa kumwaga.


Yao amesema kwa sasa atajikita zaidi kwenye muziki wake hivyo hahitaji tena mahusiano ya kimapenzi; “My babies, I am officially single, and I am going to focus on my music. Have a nice weekend,” ameandika Yao.


Kapo hiyo ilitrendi Afrika nzima baada ya kuanika mahusiano yao Agosti mwaka jana 2020 huku watu wakivutiwa zaidi na ufupi wa Grand P kutoka na bonge la mdada kama Yao huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai kuwa Eudoxie amejiweka kwa Grand P kimaslahi yaani analenga kuvuna mkwanja.


Licha ya maneno hayo, lakini wapenzi hao waliendelea kusisitiza kuwa wanapendana licha ya utofauti wao wa vimo na muonekano wa maumbile lakini wataendelea kuishi katika mahusiano yao na walipanga kufunga ndoa mwaka huu.


Grand P alizaliwa akiwa na matatizo ya kimaumbile (genetic disorders) ambayo yameathiri maumbile yake lakini hakukata tamaa, amekuwa mpambanaji na juhudu zake zimemfanya kuwa staa wa muziki na uigizaji Barani Afrika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top