Simanzi na vilio vyatawala katika mwalo mkaa (mitatu) uliopo jijini Mwanza baada ya familia ya watu watatu kuzama Ziwa Victoria wakiwa wanavua samaki, huku baba na mtoto wake wakifariki dunia.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, Revocatus Magembe amesema watu hao ambao ni Raphael Jelu Mwala (60) aliyefariki pamoja na mwanaye Paul Raphael (30) wakiwa manusura wa ajali hiyo, Bakari Mnyama (28) ambaye ni mpwa wa Raphael walipata ajali hiyo baada ya mtumbwi wao kusukumwa na upepo mkali na kuzama.
Magembe alisema tukii hilo limetokea alfajiri ya kuamkia Julai 26, mwaka huu wakati wavuvi hao watatu wakiendelea na shughuli zao.
“Wote ni wakazi wa Mtaa wa Shede kata ya Mkuyuni Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,”amesema
Jeshi hilo lilifanikiwa kuopoa mwili wa Raphael majira ya saa sita mchana huku mwili wa mtoto wake ukiopolewa majira ya saa tisa kasoro za mchana jana na kupelekwa kuhifadhiwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mwanza ya Souko Toure.
Mtoto wa kaka yake na marehemu (Raphael Jelu), Oliver Fredy alisema baba yao alikuwa amepumzika kufanya shughuli za uvuvi kwa muda wa mwezi mmoja akiwa anamalizia ujenzi wa nyumba yake, lakini siku ya tukio mtoto wake alifika saa 11 alfajiri kuchukua zana za uvuvi ndipo baba yake akaamua kwenda naye ziwani