SIMULIZI-NATAMANI NIFE LAKINI BADO SIJAITWA BABA—SEHEMU YA NANE

0


(ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA; Baadaya kuachana na Jack George anaachana kabisa na wanawake, anakua ni mtu wa mitandao kuanngalia picha za uchi na kudanganya wanawake kwenye mitandao kuwa atawao. Ghfla anashangaa Binti anakuja ofisini kwake, alimuahidi kumuoa na kaacha kazi kwajaili yake, unafikiri nini kitatokea? ENDELEA…)

Soma Sehemu zilizotangulia>>>>>1-7

Salome alikua kama mtu aliyechanganyikiwa, aliniambia hahitaji kitu chochote kile katika maisha yake zaidi ya kuwa na mimi. Dakika mbili tu alianza kunionyesha meseji nilizokua nikichart naye, kweli niliziona na ni mimi nilikua nikimjibu mambo ambayo hata sikuyajua. Ni kweli nilimuambia nitamuoa, nilimuambia aache kazi kuja kuishi na mimi na nilimuambia mambo mengi sana lakini sikumaanisha.


Nia yangu ilikua ni yeye kuendelea kunitumia picha za uchi na sikua hata na mpango wa kuja kuonana naye achilia mbali kumuoa na kuishi naye kama mke wangu.

“Dada yako ndiyo kanielekeza kwako, nilimtafuta akaniambia kuwa unafanya kazi hapa naweza kuja….” Aliniambia, ni kama alizidi kunichanganya kwani kumtaja Dada yangu ilimaanisha kuna mambo mengi ambayo walishaongea kuhusu mimi. Dada yangu alikua anataka mimi kuoa na nina ihakika angefanya kitu chochote kile ili mimi kuwa na mwamnamke.


Nilitaka kuongea naye na kumkataa palepale ofisini lakini nilijua isingesaidia, kwa hali yake angeleata vurugu na tusingeelewana kabisa. Nilirudi naye nyumbani kishingo upaende, sikua na mwanamke nyumbani hivyo sikua na kitu cha kuhofia, nilijua tu baada ya muda ataondoka mwenywe lakini haikua hivyo, siku ya kwanza, siku ya pili wiki mwezi na mwaka uliisha huku bado nikiishi na Salome.


Mwanzo niliona shida lakini baaadaye nilizoea, alikua ni mtu mzuri, binti mwenye akili ya maisha lakini alionekana kutendwa sana kwenye mahusiano, aliumizwa sana kiasi kwamba kuna wakati alikua anaweza kukaa analia mwenyewe hukua kitetemeka kama vile kamwagiwa maji ya baridi.

“Wanaume, wanaume si watu wazuri, niambie G wangu kuwa hutaniacha, niambie kuwa hutaniacha.” Aliniambia mara kwa mara na mimi nilimuambia kuwa siwezi kumuacha kwani nampenda sana.


Nadhani hali yake ilinikumbusha hali yangu, mimi pia nilikua nimeumizwa, maumivu ambayo yalinifanya kuchukia wanawake, yalinifanya kuwa na hasira na kufanya mambo yana kishenzi.

“Inamaana hutaki kufanya mapenzi na mimio au mimi ni mbaya namna hiyo?” Siku hiyo Salome aliniuliza, ulikua umepita mwaka mzima bila kukutana kimwili, tulikua tunaishi pamoja kama mke na mume lakini nilikua sijawahi kumgusa. Si kama nilikua sitaki bali nilikua siwezi, mwanzo nilikua nikimdanganya kuwa nasubiri tuzoeane, nikamuambia kuwa ninaumwa lakini siku hiyo aliingia bafuni na kunikuta nikijichua.


Alilia sana na kudhani kuwa namdharau, namuona kama si mwanamke ndiyo maana naishi naye kama dada yangu huku nikijichua. Ni hali ambayo hata mimi iliniumiza sana, baada ya kuonana na Salome niliamua kubadilika,. Nilipunguza kutumia muda mwingi kwenye mitandao na kuwa nayeye. Ingawa sikuacha kabisa lakini nilipunguza sana kwani nilikua na hamu sana ya kutengeneza familia lakini ni kitu ambacho hakikuwezekana.


Nilikua nikitamani kufanya naye mapenzi lakini kila nikimgusa hisia zilikua mbali, nilishindwa kabisa. Kuna wakati nikimuangalia makalio yake nilikua nikisisimkwa lakini nilikua namheshimu sana, nilikua sitaki kumuingiza katika hiyo dhambi pia hata mimi nilitaka kuacha. Nilijua kama nisipoacha nikianza kufanya naye basi utakua ni mchezo wangu wa kila siku. Siku hiyo alilia sana ndipo nikaamua kujikaza ili nifanye naye mapenzi.


Kusema kweli nilishindwa, nilijaribu kila kitu hata kumshika makalio lakini bado nilishindwa. Akili yangu ilishahamia kwenye kujichua na uume ulikua umelegea tu. Huwezi amini hata kwenye kujichua nako ilikua ngumu, yaani kuna wakati nilikua nikijichua lakini nuume hausimami au sifiki mwisho.


Niliona kama maisha yangu yameisha, nilijiona kama nimekufa, kila kitu kilisimama kwangu. Kushindwa kabisa kufanya tendo la ndoa kulinipa hasira nyingi sana kulinipa mawazo, kila nikirudi nyumbani nilikua mtu wa kutukana, mtu wa kumdhalilisha sana yule binti.

“Huna akili wewe, ulikuja na kunikuta na maisha yangu, nina furaha umekuja kuniloga. Wewe ni mbaya, sura mbaya kwanza unanuka ndiyo maana siwezi kufanya mapenzi na wewe, mbona nikiwa na wanawake wengine naweza kufanya vizuri, kwanini kwako nisindwe!”


Nilimtukana, yalikua ni maneno yangu ya kila siku kwa Salome, yeye alikua akiishia kuomba msamaha lakini hakuondoka. Kichwani nilijua kabisa hajanikosea kitu chochote, lakini niliamini kua, kama nikimuacha akahisi kuwa tatizo ni langu basi ataondoka na kunitangaza huko mitaani kitu ambacho sikua tayari kukiona.


“Nitakakuja kwenu, nataka kuja kukuoa, unajua kuna kitu nimekaa nikafikiri, naamini hii hali imekuja kwakua sisi si wana ndoa,. Hatujahalalisha mahusiano yetu. Najikuta nakua na wasiwasi kufanya mapenzi na mwanamke ambaye si mke wangu, naomba tuingie kwenye ndoa labda kila kitu kitabadilika.” Nilimuambia siku moja, nilifikiria sana na kuona kama nitaaibika, nilishajau hakuna uwezekano wa kupona kwani nilishaanza kutumia dawa za nguvu za kiume nyingi tu lakini sikuona mabadiliko yoyote.


“Siwezi kufa kwa aibu, hapana, mimi ni mwanaume lazima niwe na mke, kwa umri wangu ni bora kua na mke kuliko kuaibika kuwa sina nguvu za kiume!” niliwaza, lakini Salome niliona kama kabadilika, mwanzo wakati anakuja kwangu alikua kama chizi, nilikua namfanyia mambo mengi mabaya lakini alikua anavumilia na kila siku alikua ni mtu wa kuniambia kuwa anataka ndoa na mimi, alitaka niongee na ndugu zake na alitaka niende kwao kujitambuilisha.


Wakati huo nilikua naringa ila siku nilipomuambia kuwa nataka kumua aliisita kidogo.

“Mbona haraka hivyo?” Aliniuliza, lilikua ni swali la kawaida ambalo mara nyingi mimi ndiyo nilikua nikimuuliza alipokua ananiambia kuhusu ndoa lakini aliponiuliza nilihisi kama kasema hapana, hanitaki mimi si mwanaume, nilijikuta napaniki na kuona kama ananiacha, sijui ni kitu gani kilitokea lakini nilinyanyuka harakaharaka nikachukua simu yake nikamuambia aifungue password lakini aligoma, hapo ndipo alizidi kunichemsha kwani nilihisi kabisa anachepuka na ana mwanaume mwingine.


Huko mwanzo hakua msiri kihivyo na sikua nikimfuatilia kwani niliona kama hana pakwenda, mwanamke mwenyewe amejileta kwangu ni kwanini nihangaike naye. Aligoma kufungua simu nikaanza kumpiga, nilimpiga sana lakini aligoma, kila nilivyokua nikimpiga na kumtukana ndivyo ambavyo nilijisikia vizuri, nilijisikia mwanaume na nilitamani kuendelea kumpiga.


Yeye aliishia kuomba msamaha, lakini katika kupigana alinisukuma kidogo nikadondoka hapo ndipo alipata upenyo na kutoroka, alikimbia, alirudi na Polisi na kuchukua vitu vyake, wakati anaondoka aliniambia kua hawezi kua na mimi kwani ana mimba ya mtu mwingine na mimi si mwanaume.

“Tafuta msaada…” aliniambia, nilijisikia vibaya, ingawa hakuongea kwa nguvu watu wakasiikia lakini namna alivyoniacha ni kama alikua ananionea huruma, ni kama alikua ashanichoka muda mrefu naye alikua akitafuta sababu ya kuniacha.


“Kama huyu naye akniacha mimi nitakua mgeni wa nani?” Niliwaza wakati anaondoka si kama nilimpenda Salome lakini nilimuona naye kama mtu aliyechanganyikiwa, mtu mwenye hamu sana ya mwanaume hivyo nilimini kuwa atanivumilia pamoja na matatizo yangu. Aliniacha nikiwa na huzuni sana, nilishindwa hata kuenda kazini, nilijisikia vibaya.


“Mbona nilikua kijana mzuri, nilikua na nguvu zangu za kiume nyingi tu, nilikua napendwea na wanawake, nilikua na maisha yangu nini kimebadilika?” Niliwaza sana bila kupata majibu, nilianza kujichukia, nilianza kuyachukua maisha na kutaka kufa kabisa. Nilishatumia dawa nyingi za kuongeza nguvu za kiume bila mafanikio, nilishafanya kila kitu bila mafanikio, sikuweza hata kujichua, hata uume ulikua kama haushtuki tena.


“Nini hiki, inamaana ndiyo maisha yangu yamekua hivi? Inamaana siwezi kupata mtoto tena?” Niliwaza bila majibu, nilikua naumia sana nikiona rafiki zangu wakiwa na watoto, swali la unaona lini lilikua likiniumiza sana. Ndugu waliongea wakachoka lakini sikuwa na uwezo wa kufanya mapenzi na mwanamke na hali hiyo ilinifanya kuogopa sana kuwasogelea wanawake nikiamini kuwa watanitangaza.


Nimekua mtu wa hasira, nimekua mtu wa kudhalilisha wanawake kwenye mitandao na mabaa medi, nawalipa ili kuwashikashika na kuwahdalilisha najikuta nawapiga bila sababu. Nimerudi kwenye kunywa pombe na kuchart na wanawake, wakinitumia picha za uchi basi nafurahi jinsi wanavyodhalilika. Wake za marafiki zangu ambao wananiona kama kijana mzuri, wanajilengesha natumia pesa naishia kuwapiga picha za uchi na kutuma kwenye magroup ya Telegram.


Mwanzo nilikua napata raha nikiona wanadhalilika, nikiona rafiki yangu kaona picha za uchi ambazo mke wake kanitumia kwenye mitandao basi najisiki raha sana, ile hali ya wao kukosa amani nahisi wanakua kama mimi lakini sasa hivi sina raha tena. Nimechoka na haya maisha, natamani kufa, sitamani kuishi tena, natamani nisiwepo, natamani kufa lakini bado sijaitwa Baba sijui nifanye nini kwani sioni tena sababu ya kuishi.


Natamani uandike kisa changu kwani mara nyingi unaandika kuhusu wanawake, wapo wanaume ambao tumeumizwa, wapo ambao bado tunabeba maumivu ya zamani, wapo ambao maumivu yameafanya kuwa wanyama kama mimi. Nimefanya mambo mengi mabaya na yote ni kutokana na hasira za X wangu, nilimpenda lakini hakuonyesha kunijali na kila nilivyozidi kumpenda ndivyo aliziodisha maumivu.


Mpaka sasa hajaondoka kichwani kwangu, nikiongea na mwanamke namuona yeye, nikimuona namna alivyo na furaha kwneye mitandao ya kijamii natamani kumfuta kumpiga lakini nilishajaribu nikishamuona nakua kama mtoto mchanga, nakua sina nguvu tena ya kufanya chochote.


Nachukua mwanamke mwingine ambaye hata siwezi mfanya chochote namlewesha na kuishia kumpiga, kweli nimechoka natamani sana kufa lakini sina mtoto, sijui hata nifanye nini, niemchoka hii hali ya kudhalilisha wanawake? Nafanya kazi nzuri lakini maisha yangu hayana thamani tena kwani nyumbani siheshimiki, kazini nadharaulika, wananiona mlevi wananiona kama nimechanganyikiwa na kwakua tu sijaitwa Baba na siwezi kuoa.


MWISHO

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top