TAARIFA MPYA KUHUSU VIFO VYA WANAFUNZI,WALIOFUKIWA NA KIFUSI.

0

 


HABARI WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Mbori wilayani Mpwapwa wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi walipokuwa wakichimba mchanga kwenye korongo.


Inadaiwa kuwa wanafunzi hao walitumwa mchanga huo na walimu wao.


Akizungumzia tukio hilo leo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Josephat Maganga, amesema tukio hilo limetokea saa tatu asubuhi na limeacha maswali mengi ya kujiuliza.


Amewataja wanafunzi waliofariki ni Rehema Alex ambaye anasoma darasa la nne, Daudi Machea wa darasa la tano na Ezla Lucas wa darasa la sita.


Waliojeruhiwa Arafa Athumani(10), Nelly Daudi(12), wilsoni Amosi, Yunis Mussa(12), mwijuma machimo(13),


“Kuna maswali ya kujiuliza walienda peke yao? nani aliwatuma? Je, ilikuwa ni wakati wa vipindi vya darasani? Kuwatuma mchanga kwenye mto na kokoto tumepiga marufuku,”amesema.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top