➡UZI FAHAMU HAYA KUHUSU AFYA YA AKILI

0


Kabla ya yote usisahau KUALIKA WATU WAJE KUTEMBELEA MTANDAO HUU TUTAKUELIMISHA KILA NYANZA  ILI darasa lifike mbali, utakuwa umeonyesha kuwa na Afya Imara sana ya Akili 😄😄. 

●Afya ya akili:

Ni ustawi wa fikra, tabia na hisia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku. 

KWANINI UIFAHAMU AFYA YA AKILI? 🤔

Nakupa point 7 tu, sitaki nikuchoshe msomaji wangu... 👇

●1. Kuifahamu afya ya akili huleta furaha,upendo na amani ya nafsi. Muhimu sana hii, unapoielewa Afya ya Akili inakusaidia kepuka vitu vinavyoweza kukuondolea furaha, upendo na amani, Mfano Hasira na chuki.


●2. Kutambua wakati sahihi wa kupata msaada wa kisaikolojia.

Ni rahisi mtu anayefahamu afya ya akili kugundua wakati ambao hayupo Sawa kiakili na kutafuta huduma ya kisaikolojia na kumuepusha kufanya maamuzi mabaya yanayoweza athiri maisha yake.

●3. Kuweza kutambua changamoto ndogondogo ambazo zaweza kupelekea tatizo la akili.

Mfano, msongo wa mawazo usipopatiwa ufumbuzi hupelekea tatizo la akili liitwalo Sonona.


●4. Kuitambua afya ya akili kunasaidia kupambana na shida ya kiwewe (Post traumatic stress problem) inayosababishwa na majanga mbalimbali.  Mfano mtu anapofiwa na mpendwa au mtu wake wa karibu

●5. Mtu mwenye ufahamu kuhusu afya ya akili itamsaidia kujua namna ya kuitunza afya yake ya akili. Mfano, kujua umuhimu wa kulala kwa ratiba ya kueleweka kuliko kulala bila mpangilio ambapo hupelekea kuathiri ustawi wa akili.●Masta unajua binadamdu anatakiwa alale kuanzia masaa 6-8 ili kuisaidia akili kua imara? 🤔. 

Sikia sasa, mtu akishindwa kulala masaa ya kutosha hupelea mlundikano wa sumu mwilini na pia kupelekea baadae tatizo la akili kama vile ugonjwa wa kusahau (insomnia).
 Ishi nayo hiyo ✍️

● 6. Familia yenye uelewa mzuri wa afya ya akili kutasaidia watoto kulelewa vizuri na wazazi wao kiakili na kimwili, mfano kutambua tabia za watoto, kuwapa watoto uhuru wa kuchezakujieleza, kujifunza, kuwapa upendo, kuvitambua na kuviendeleza vipaji vya watoto.

●7. Uelewa wa afya ya akili utasaidia kupunguza matatizo ya kikatili na uzalilishaji ndani ya jamii.

Elimu ya afya ya akili inasaidia kuwasaidia wanajamii wote kulinda afya zao za akili na za wenzao baada ya kujua madhara ya kuwafanyia wengine masuala ya ukatili na udhalilishaji 

●Afya ya akili na Maendeleo katika jamii huwezi zitenganisha..

Kupata madini mengi kuhusu Saikolojia ,Teknolojia , Mahusiano, Maendeleo binafsi, Biashara na mengine mengi yanayo gusa maisha ya kila siku

We alika tu watu kupitia hii kupitia Icon za mitandao ya kijamii hapo chini! Tuwe wengi pamoja.
Imeandaliwa na Cylas wa kwanza
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top