✒UZI-JE WAJUA KWANINI WAKILI NA MWANASHERIA NI WATU WAWILI TOFAUTI?

0

Karibu msimaji wa UZI kupitia mtandao wetu was Idawa Blog,karibu kwanza tuanze kwa kujua maana ya maneno haya mawili wakili na Mwanasheria ni kina nani kisha tuendelee karibu.

● MWANASHERIA NI NANI

Mwanasheria ni mtu yoyote yule ambaye ana elimu ya sheria, elimu hyo inaweza kuwa ngazi ya cheti, diploma au degree au masters . Maana yake kuwa mtu huyu ana ujuzi juu ya mambo ya sheria.

● WAKILI NI NANI

Wakili ni mtu yoyote ambaye ana elimu ya sheria na ambaye amemaliza kwa kufaulu shule ya mafunzo kwa vitendo ya sheria " *LAW SCHOOL* " kisha kuhudhuria interview kwa Jaji Mkuu na kuapishwa na Jaji Mkuu.

Wakili lazima aapishwe na Jaji Mkuu.


●Wakili lazima apewe namba ya utambulish9 na Jaji Mkuu ,namba hiyo ndo inakua utambulisho wake wa uwakili na jina lake litaingizwa kwenye orodha ya mawakili iliyopo pale pale kwa msajili wa Mahaka Kuu.

Zamani kulikua hakuna shule ya vitendo ya sheria badala yake watahainiwa.

●Walikua wanafanya Bar exam kisha ukifaulu ndo unaapishwa kuwa wakili.

Kwa sasa Law School kuna mitihani isiyopungua 20, ili uweze kuapishwa kuwa wakili unatakiwa kufaulu mitihani yote hiyo.

 


● MIHURI YA WAKILI 

Wakili akishaapishwa anakua na mihuri 2.

 1. Kuthibitisha Nyaraka kuwa ni halisi

2. Kuapisha

Wakili anakua na cheo cha kamishina wa viapo  anaweza kumuapisha mtu juu ya jambo fulani ,ndo maana Affidavit zinatengenezwa na kusainiwa na wakili.


●Ukiwa na nyaraka ambayo ni kopi na unataka kwenda kuitumia sehemu basi mhuri wa wakili haukwepeki hapa.

Ukiwa unataka kuthibitisha kuwa maelezo unayotoa ni halali na kweli basi mhuri wa Wakili haukwepeki hapa.

Gharama za mihuri zimewekwa kisheria.


●TOFAUT YA WAKILI NA MWANASHERIA KIUTENDAJI

Mwanasheria hawez kufanya yafuatayo

-Kuthibitisha nyaraka 

-Kuapisha

-Kumuwakilisha mteja mahakamani

-Kumtetea mteja mahakamani

-Kutengeneza Nyaraka

Wakili anaruhusiwa kufanya hayo yote ambayo Mwanasheria haruhusiwi.


●UNAWEZAJE KUMJUA WAKILI

Ni rahisi sana ingia mtandaoni andika  Mjue Wakili then utaandika jina lake pale ,Kisha majibu yatakuja kama anaruhusiwa au haruhusiw. 

Kama anaruhusiwa basi ujue huyo ni wakili na leseni yake iko hai.

Kama haruhusiwi huyo sio wakili.


●Mwisho Kila Wakili ni Mwanasheria lakini 

Sio kila Mwanasheria ni Wakili.

Asanteni wote. Unaruhusiwa kushare link kwa kutumia icon za mitandao ya kijamii hapo chini!.

Imeandaliwa NA Cylas wa Kwanza


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top