Leo tupo na LINKEDIN
LINKEDIN ni mtandao wa zamani sana, kabla hata ya Facebook, linkedin ilianza takribani miaka 18 iliyopita, namaanisha mwaka 2003 ndio Linkedin ilianza RASMI.
Na mwanzilishi wake huyu, Bwana Reid kabla hajaianzisha Linkedin alikuwa katika Bodi ya wakurugenzi wa Google, Ebay na Paypal..
Kwahiyo huyu mtu bhana alikua karibu sana na maswala la mitandao kabla hajaanzisha mtandao wake huo..
Kwahiyo Linkedin sio ya kitoto ni mtandao mkongwe sana kuliko Facebook ambayo ilianzishwa mwaka 2004, au twitter iliyoanzishwa 2006, au huyu mtoto Instagram aliyeanzishwa 2012.
kwasasa Linkedin ina watumiaji zaidi ya milioni 740 Duniani kote. Na ikiwa inatumika kwenye nchi zaidi ya 200 duniani.
Unaambiwa kwamba Linkedin ilikua inakua kwa shida sana, katika mwezi wa kwanza wa kuanzishwa kwake ilifanikiwa kupata watumiaji 4500, lakini badae wakawa wanajiunga kwa wastani watu 20 kwa siku, hii ni takwimu mbaya sana kwa ukuaji wa mitandao ya kijamii.
Kwa Tanzania Linkedin inakua taratibu na kwasasa una watumiaji zaidi ya Milioni Moja. Unataka kukaribiana na mtandao wa Instagram ambao una watumiaji zaidi ya milioni Mbili Tanzania
Shida ni moja tu ambayo inaufanya haufahamiki sana ni kwamba Hauna Kelele kama zilivyo Instagram na Youtube.