Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Geita kwa kushirikiana na askari wa GGM wamedhibiti moto uliowaka kwenye moja ya darasa la Shule ya sekondari Geita iliyopo mjini Geita.
Moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana umeanza kuwaka saa 3 usiku na kuteketeza magodoro na masanduku ya wanafunzi yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye chumba hicho.
Soma zaidi>>> Mwananchi digital