Wananchi Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbalizi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Mkoa wa Mbeya wamelalamikia vitendo vya ubakaji vinavyofanywa na mmoja wa wafanyabiashara wa Mtaa wa Mbalizi.
Kwa mujibu wa madereva na wafanyabaishara wa karibu na mtuhumiwa wamedai imekuwa ni kawaida kwa mtenda, kutenda vitendo hivyo kwa mabinti wengi wakiwemo wanafunzi kwa muda mrefu hali iliyowachosha majirani na kumtaka kuhama kufanya biashara katika eneo hilo.
Wanasema mtuhumiwa huwarubuni mabinti wadogo wanaotembeza biashara zao na kuahidi kununua bidhaa zote ili mradi tu amuingize kwenye mtego wake ambao mwisho wa siku huishia kuwafanyia udhalilishaji.
Ulrich Matei kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Steven Mbando ambaye kwa sasa yupo mikononi mwa jeshi la Polisi.
Tangu miaka ya 2017 Mji wa mbalizi umekuwa ukitajwa kuwa na ongezeko la wimbi la ubakaji,ulawiti na mauaji, matukio yanayohusishwa na imani za kishirikina huku idadi kubwa ya matukio hayo yakidaiwa kutekelezwa na wafanyabiashara.