Wananchi wa eneo la Lusanga kata ya Kwamagome wilayani Handeni mkoani Tanga,wameandamana na kuzuia msafara wa mkuu wa wilaya wakati anaelekea mgodi wa Dhahabu wa Mamgambazi ili kushinikiza kupatiwa eneo kwajili ya kujenga shule na kufunguliwa njia ya mifugo. Tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu asubuhi ambapo zaidi ya wananchi 150 walijitokeza na kufunga barabara ya kuelekea Morogoro kuzuiara msafara wa mkuu wa wilaya na aliposimama wamesema shida yao ni kupatiwa eneo kwaajili ya ujenzi wa shule lakini pia kufunguliwa njia ya mifugo kwenye eneo ambalo amepewa muwekezaji bila wao kushirikishwa.
Tazama video kilichoamuliwa na mkuu wa wilaya.