WANAODAIWA WAPENZI WAKUTWA CHUMBANI WAMEFARIKI DUNIA.

0

 


Watu wawili wamefariki dunia mkoani Njombe baada ya kuingia na jiko la mkaa katika chumba cha kulala kwa ajili ya kupunguza baridi.

Hayo yalibainishwa leo Jumatano Julai 21, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi hilo mkoani hapa.

Alisema marehemu hao waliokutwa na umauti walifahamika kwa majina ya Benitho Mbatha (23) mpiga debe wa mjini Njombe na Jazila Said ambaye kabila ni Mndendeule (27) mkazi wa Namtumbo mkoani Ruvuma.

“Baada ya kufariki hakuna mtu ambaye aligundua kama kuna watu wamefariki, tukio hili limetokea tarehe 17 mwezi wa saba majira ya saa tano na nusu huko mtaa nwa National Housing kata ya Njombe mjini wakiwa wamelala kwenye chumba kimoja,”alisema Issah.

Alisema sababu ya kifo chao inaonyesha wakati wakiwa hai waliweka moto wa mkaa kwa ajili ya kujihifadhi na baridi ambapo mtindo huo umekuwa ukitumika na watu wengi mkoani Njombe.

Aidha Kamanda Issa alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe kutumia njia nyingine kujikinga na baridi na si kuota moto kama ambavyo wengi wamekuwa wakifanya kwa kwani kufanya hivyo ni hatari kwa maisha yao.

Read more>>>>>>>

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top