WEKA MIPAKA YA MAZOEA NA WANAUME KWANI UKIFUNGUA MILANGO WAO WANAINGIA TU!

0


Kuna mume wako na kuna yule mwanaume ambaye ukiongea naye unajisikia raha. Hakufanyii chochote lakini mmezoea kuchekacheka naye, anakusaidia vitu vidogo vidogo kiasi kwamba kuna wakati ukikaa bila kuongea naye siku mbili tu unammisss na unahisi kuchanganyikiwa flani hivi.


Huyu unamchukulia kama rafiki hivi na inawezekana mume wako anamjua na anawajua kuwa ni marafiki. Lakini kama unaona kuwa mazoea yamezidi, mnatumiana mpaka meseji za mapenzi, mnaongea mambo ya chumbani na huyo mwanaume basi huu ndiyo wakati wakupunguza mazoea na kukata kabisa mawasiliano na huyo mwanaume.


Narudia, anakuondolea upweke lakini kama mshaanza kufanya mambo ambayo, mwanaume wako akikuona anahisi mnachepuka, kama hakuna mipaka tena ya heshima, anaweza kuja kukushikashika tu, kukuchezea wakati wewe ni mke au mpenzi wa mtu basi ni wakati wa wewe kukata mazoea.


Labda nikuambie kitu kimoja, sisi wanaume hatuoni kama ni shida, yaani kuwa na mwanamke wa namna hiyo, hutembei naye lakini unamtania, na kama akikuacha basi unaweza kumshika popote na hajali, kama ukimpigia simu mnaweza kuchart chochote, kama mapicha ya hovyo ya kwenye mitandao mnatumiana wanaume hatujali na hatuna mipaka.


Wanaume hatujali tunapomfanya kwa wake za wengine au wa penzi wa wengine. Lakini sasa, yayeyale unayofanya na mfanyakazi mwenzako ofisini ukisikia au ukiona mke wako anafanya ni ngumu sana kwanza kukubali kuwa ni utani tu hakuna mapenzi na pili kusamahe na kusahau. Kwa maana hiyo, dada zangu, ni lazima wewe kujiwekea mipaka.


Kama umeolewa au una mwanaume ambaye unampenda au hata kama huna, weka mipaka ya mazoea na mwanaume ambaye si wako. Asikushikeshike tu kwakua nyie ni washikaji, asikutumie mameseji yasiyoelekweka, mambo ya baby, sweteee sijui na vitu kama hivyo. Mume wako anaweza kuwa na Roho ya kizungu ila kama ni hii ngozi yetu nyeusi ni ngumu sana kumuelewesha! Weka mipaka wewe, amka, punguza mazoea!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top