Adaiwa kujinyonga baada ya kubainika na maradhi ya UTI

0

 


Akizungumza na Nipashe jana, Diwani wa Usisya, Aziza Galula, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai, kuwa Veronica aliacha ujumbe wa kuwaaga wazazi wake na kuelekeza fedha zake za mauzo ya tumbaku zikilipwa, apewe mama yake.

Alisema tukio hilo lilitokea Julai 30, mwaka huu, katika kijiji hicho majira saa 10 jioni, baada ya kutoka zahanati ya kijiji hicho kupima afya yake.

Diwani huyo alisema kuwa kabla ya kutokea kwa tukio hilo, Veronica alikuwa akisumbuliwa na homa na kwamba baba yake, Tadeo Joseph, alimpeleka kwenye vipimo na waliporejea nyumbani aliamua kuchukua uamuzi huo.

"Alikuwa anaumwa japo hali yake haikuwa mbaya sana, baba yake akampa dozi ya mseto, lakini haikumsaidia na baada ya hapo waliamua kwenda zahanati ya hapa kijijini, alipopimwa alikutwa na U.T.I," alidai diwani huyo.

Alidai kuwa wamebaini binti huyo alijiua kwa kunywa vidonge vyote alivyopewa hospitali na baadaye kujinyonga nyuma ya nyumba yao, huku akiacha ujumbe.

"Baba na mama nimeamua kujiua, ninawatakia maisha mema. Pia kuna hela ya tumbaku ikitoka, basi hela zote achukue mama," ulisomeka hivyo ujumbe unaodaiwa kuandikwa na Veronica kabla ya umauti kumfika.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ukondamoyo katika Kijiji cha Katungulu, Selemani Kapaya, ambaye ni jirani wa familia hiyo, alisema wamesikitishwa na tukio hilo na kutoa ushauri kwa wananchi wa kitongoji chake kuhakikisha halitokei tena.
Ilidaiwa kijijini huko kuwa, Veronica alikuwa akijishughulisha na ushonaji na kilimo cha tumbaku.

Baadhi ya majirani walisema binti huyo alikuwa mchapakazi na hakuwahi kuonyesha tabia mbaya hapo awali na alikuwa akishirikiana na jamii katika mambo mbalimbali na wamesikitishwa kwa kumpoteza.

Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Safia Jongo, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuwataka wananchi kuacha kujichukulia kisheria mikononi.

Aliwataka wazazi kutekeleza kikamilifu wajibu wao wa msingi wa kukaa na familia zao na kusikiliza shida zinazowakabili vijana wao na kuzipatia majibu.

Alisema wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho na baada ya upelelezi, kukamilika watatoa taarifa ya kiini cha kifo hicho japo hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na jeshi hilo kutokana na tukio hilo


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top