Adaiwa kujinyonga kisa ugumu maisha

0

 Kwa mujibu wa taarifa za ndugu na majirani zilizothibitishwa na mamlaka husika za ulinzi na usalama ngazi ya mkoa, Likange aliondoka nyumbani kwao Agosti 3, mwaka huu na hakuonekana tena hadi Agosti 7, mwaka huu majira ya mchana mwili wake ulipokutwa unaning'inia kwenye mti eneo la makaburi.Majirani hao wakiwamo Yusuf Juma, Kindamba Hemedi, Lucy Joseph na mama mzazi wa Likange, walidai kuwa mwili wake ulikutwa unaning’inia juu ya mti wa mkorosho eneo la makaburi ya Mtaa wa Nangando mjini Liwale ukiwa umeharibika.

“Baada ya kumtafuta takribani kwa siku nne, hatimaye tukaukuta mwili wa Faraji ukining’inia juu ya mti wa mkorosho.
"Wamesema kupatikana kwa mwili huo kulitokana na harufu iliyokuwa ikisikika ya kitu kilichooza kutoka eneo la makaburi yaliyopo Mtaa wa Nang’ando," alidai Juma.

Mashuhuda hao walisema kuwa kutokana na mwili kuharibika, mara tu baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa wataalamu wa afya na Jeshi la Polisi, wananchi walichimba shimo usawa ulikokuwa unaning’nia mwili huo kisha wakakata kamba na kuufikia mwili huo.

Walidai kuwa Likange alirejea mjini Liwale mwishoni mwa mwaka jana, akitoka Gereza la Mtwara kutumikia kifungo kwa kosa la ubakaji.

Ilidaiwa kuwa baada ya kutoka gerezani, Likange alionekana mnyonge ya kutokuwa na furaha, akisikika akidai hali ya maisha ya uraiani kwa upande wake kutokuwa rafiki.

Mama wa Likange, Darini Ngambe, aliiambia Nipashe kuwa tangu kijana wake arejee nyumbani kutoka gerezani, hakuwa na furaha na mara nyingi alionekana mnyonge, akilalamika hali ugumu wa maisha uraiani.

Alidai kuwa wakati anaondoka nyumbani wiki iliyopita, hakumuaga mtu yeyote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi, akizungumzia tukio hilo, athibitisha kuwapo kutokea na kukiri kwamba Likange aliwahi kuhukumiwa kutumikia kifungo gerezani kwa kosa la ubakaji.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top