Mwanamke ambaye alimuibia mwajiri wake simu yenye thamani ya KSh 40,000 mjini Nairobi na kumupa mpenzi wake, amefikishwa kortini pamoja na jamaa huyo.
Rebecca Isiche Elumbe anasemekana kuiba simu, seti tatu za mikufu ya dhahabu zenye thamani ya KSh 300,00 na KSh 90,000 kutoka nyumbani kwa makazi ya Abdi ya Royal Park Estate mtaani Langata, Nairobi nchini kenya
Kwa mujibu wa ripoti ya Nairobi News, Elumbe alitoroka kwenda nyumbani kwa mpenzi wake ambapo alimupa simu hiyo na KSh 1,000 kabla ya kusafiri hadi kwao mjini Eldoret siku moja baadaye.
Abdi alieleza kuwa kijakazi wake alikuwa ametoweka na wakati alirejea nyumbani akitokea hospitalini mtaani South C , alitambua kuwa kijisanduku ambacho alikuwa ameweka vitu hivyo vya thamani hakikuwepo.
Ilimbidi kuripoti haraka katika Kituo cha Polisi cha Lang'ata na cha Eldoret kilichoko karibu na nyumbani kwa mshukiwa.
Hata hivyo mshukiwa alikamatwa na pia kuwaongoza polisi hadi nyumbani kwa mpenzi wake ambaye akipatakaa na simu hiyo.
Wakifika mbele ya hakimu mkuu Phillip Mutua katika Mahakama ya Kibera, Agosti 9, wapenzi hao walikubali mashtaka ya wizi dhidi yao.
Chanzo:Tuko swahili