Polisi katika kaunti ya Bomet wameanzisha uchungizi kuhusu kisa ambapo mwanamume mmoja anadaiwa kumumwagia mke wake chai moto kwenye sehemu zake za siri na miguu baada yake kusoma jumbe za mpenzi wake wa kando.
Akizungumza na wanahabari Jumapili, Agosti 29, mwathiriwa Sharon Chepkorir, 25, alielezea kuwa mume wake alimfumania akiandika chini nambari ya simu ya mpenzi wake wa pembeni.
"Aliniona nikiandika chini hizo nambari kisha aliniuliza nilikuwa nafanya nini na simu yake lakini nilinyamaza.
Ni katika harakati hiy ndipo alichukuwa chai kwa moto na kunimwagia," alisimulia. Katika video ya The Standard, Sharon anauguza jereha la kuchomwa kwenye mguu wake wa kushoto na anaonekana kushindwa kutembea.
“Nilichomwa sehemu zangu za siri na sehemu ya miguu yangu na mapaja.
Siwezi keti vizuri," alisema huku akilia.
Ndoa yao imekuwa ya vita Kulingana na mmoja wa jamaa za mwathiriwa, David Yegon, wanandoa hao wamekuwa wakitofautina kila mara na hata kushindwa kusuluhisha tofauti zao.
“Tumejaribu kutatua masuala haya mbeleni kama familia, na ninafikiri wakati umefika maafisa wa serikali waingilie kati," alisema Yegon.
Ujumbe uliozua mkasa Ripoti zinadai kuwa mshukiwa Alfred Kigen, mwenye umri wa miaka 32, alikuwa amepokea ujumbe uliosoma "mambo" kutoka kwa mmoja wa mahawara wake.
Chifu wa kata ya Chemelet, Evans Maritim alithibitisha kisa hicho na kusema uchunguzi umeanzishwa na maafisa wa polisi kubaini chanzo chake. Kwa sasa Sharon ametibiwa na yuko buheri wa afya.
Chanzo:Tuko News