AMENIACHA KWAKUWA NIMEMSADIA X WANGU NIFANYE NINI ?

0

 


Nashindwa kuelewa  nifanye nini ili mume wangu anisamehe, mimi ni Mama wa mtoto mmoja, nilbeba ujauzito kabla ya ndoa lakini mwaka jana mwishoni nilifunga ndoa na mume wangu. Kabla ya kuwa kwenye mahusiano na mume wangu kuna mwanaume ambaye nilikua naye lakini tukaja kuachana yeye akaoa mwanamke mwingine.


Lakini baada ya muda alinitafuta na kuniambia kuwa yeye na mke wake hawako vizuri wanagombana mara kwa mata, kwakua alishaoa nilimuambia kuwa mimi siwezi kuwa mchepuko wa kila siku hivyo aendelee na maisha yake. Lakini pamoja na yote hayo bado aliendelea unitafuta na kuniambia basi ntuwe marafiki, kwakua ni mtu niliyekua nampenda na hatukuachana kwa ubaya basi nilikubali.


Alikua kama rafiki yangu, yeye ni mtu wa kunishittikisha kwa kila kitu, ananaimini kuliko hata mke wake hivyo alinishirikisha mambo mengi na hafanyi maamuzi yoyote bila kuniambia. Kakua ni kama rafiki basi htaa kwenye harusi yangu alichangia na nilimkaribisha, alikuja na kucheza sana,a likua amekuja na mke wake, wakati huo mke wake alikua hajui kama nilishawahi kuingia kwenye mahusiano na mume wake na wala sikua na ukaribu naye.


Lakini baada ya harusi yangu tu kila kitu kilianza kubadilika, mke wake alianza kunitafuta, kumbe kuna picha zangu alishazikutaga kwenye laptop ya mume wake, alikua bado hajazifuta na hakutaka kuzifuta. Basii aliponiona siku ya harusa inigundua ni mimi na aliumia sana kwa mume wake kumleta kwenye harusi ya x wake.


Alinitafuta na kunitukana sana lakini kwakua mimi sikua na kitu na mume wake nilimuambia wakamalizane wenyewe. Mwanaume kujua kuwa kanitukana basi alinitafuta na kuniomba msamaha akaniambia anajuta sana kumuoa yule mwaname na hajui ni kwa nmna gani aliweza kuniacha na kuoa msukule kama yule. Aliongea maneno mengi sana lakini mimi nilimuambia kumheshimu mke wake, basi tangu siku hiyo nilipunguza mawaisliano lakini mwanaume hakutaka.


Alizidisha kunitafuta na kwakua mke wake alikua akiniguatilia basi alijua kuwa hatujaachana. Kumbe wakati wote huo mk wake alikua akihangaika sana kupata namba ya mume wangu, alihangaika sana mpaka mwezi wa tatu mwaka huu, wakati huo ndoa yangu ikiwa na moiezi mitatu tu, aliipata namba ya mume wangu, akamtafuta na kumuambia kuwa mimi natembea na mume wake na ni  wangu, nilimualika kwenye harusi makusudi ili kumuumiza.


Alimtumia screenshot za meseji ambazo tilikua ukitumiana na   wangu alikua akinijibu akinisifia huku akimtukana mke wake. Mume wangu alikuja kuniuliza nikamuambia ukweli kuwa mimi sina mahusiano naye, alikua ni X wangu lakini kaoa na ana maisha yake, kusema kweli mume wangu hakuniamini, pamoja na kuongea sana lakini aliniambia kama nimeachana naye miaka mitatu nyuma kanini bado nawasiliana naye.


“Hivi ungekuta meseji mimi nachart na wangu, nakuponda wewe na kumsifia yeye ungejisikiaje. Hivi ningeelika wanawake woyte niliotembea nao kwenye siku yetu muhimu ungejisikiaje? Mwanauame ulishatembea naye unamualika anakuja kukumbatia mbele yangu na siku ile yule mshenzi alikuja na kunipogeza sana unafikiri ungekua wewe ungesikiaje?” Kaka kwa namna mume wanu alivyoongea nilijisikia vibaya, niliona kama nimekosa hivyo nilikubali na kuomba msamaha kuwa siwezi kuwaisliana naye.


Mume wangu aliniambia kuwa kanisamehe, lakini hakua sawa kabisa, alikua kabadilia na tukawa hatuna amani. Niliendelea kumuomba msamaha mpaka mambo yakaisha akawa amerudi kawaida. Mambo yaliendelea vizuri, tuliendelea na mume wangu akanisamehe, lakini ji mume wangu akaudi nyumbani na kuniambia kuwa hawezi tena kuishi na mimi.Niliuuliza kwanini ndipo akanionyesha meseji nilizokua nachart na X wangu, kaka kama wiki moja nyuma X wangu alinitafuta, mimi nafanya kazi Ofisi moja kubwa hivi, alikua na shida hapo hivyo alinitafuta ili nimsaidie, nilimuambia kuwa siwezi kumsaidia lakini alisisiiza sana, basi nikakubali, kuna kitu nikamsaidia akafanikiwa. Basi kumbe nilisaau kufuta hizo meseji na wkakua hakukua na kitu kibaya sikuona sababu, lakini mume wangu kaziona na kakasiika kwanini bado naendelea kuwasiliana naye.


Nilimuambia sikuwaisiliana naye kimahusiano alikua ana shida namsaidia kama binadamu lakini hakunuelewa ume wangu alinichukua na kunilete anumbani kwetu akanikabidhi kwa Baba yangu kisha akaniambia kuwa hawezi tena kuishi na mimi kwakua aanaamini moyo wangu upo kwa mwanaume mwingine ndiyo maaana siwezi kumuacha. “Nasubiri angalau mwaka uishe nianze kuhangaikia talaka, nitalea mwanamgu”.


Mume wangu aliniambia, Kaka hajaongea kitu chochote, ananiambia hawezi kuishi na mimi tena ashidnwa kuelewa kaka kosa langu ni lipi? Hivi Kaka kuachana na mtu ndiyo iwe uadui, kwani kumsaidia X wako ni shida? Nampenda sana mume wangu lakini nashindwa kuelewa hata anachokasirikia ni nini? Sijafanya chochote na huyo kaka na tulishaachana naye nashindwa kuelewa ni kwanini mume wangu hajiamini na nifanye nini ili kurudisha ndoa yangu?


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top