ANATAKA NIUZE NYUMBA YANGU TUJENGE NYINGINE NDIYO ANIOE!

0

 

Hivi ni kweli Kaka mwanamke ukiwa na mafanikio huwezi kuolea. Mimi ni binti wa miaka 23, sijaolewa ila niko kwenye mahusiano na kijana mmoja yeye kamaliza chuo mwaka jana bado hajapata kazi, ana miaka 24, niko kwenye mahusiano naye huu ni mwezi wa tatu. Kaka huyu mwanuame ananiambia anataka kuoa mwanamke mwingine, natamani hata kufa.Mwanzo aliniambia anataka nibebe mimba yake ili nimuaminishe kama nampenda au la, kwakua nakusoma nilimuambia aje kwetu kwanza lakini alikataa na kuniambia kuwa bado hajajipanga. Wakati huo alikua anajua nauza duka la dada yangu, lakini baada ya kuanza kumpenda nilimuambia kuwa duka ni langu.


Nilimuonyesha nyumba yangu kubwa na nina Bajaji mbili. Baada ya kumuambia hivyo Kaka huyo mwanaume alibadilika sana, akawa ni mtu wa kisirani, kitu kidogo ananiambia sina akili, siwezi kuolewa na maneno kibao. Miomi nimekua nikimvumilia kwakua nampenda, sababu ya kuja kwako nikuwa, juzi kaniambia kuwa mwanamke ukiwa na mafanikio huwezi kuolewa.


Ananiambia kuwa anataka kuja kwetu kujitambulisha hivyo kama nataka kuingia kwenye ndoa naye basi tuuze nyumba yangu ili tununue kiwanja kingine na tujenge wote asimamie yeye kwani mimi ni mwanamke hivyo sitakiwa kuwa na nyumba yangu mwenyewe. Nilimuambia hapana akaniambia kuwa ni bora tuachane kwani hawezi kuoa mwanamke ambaye kamzidi maisha, anataka kuoa mwanamke mwingine mwaka huu huu kama sitakubali.


Kaka nilihisi kuchanganyikiwa kwani nampenda sana na anaonekana kunipenda. Hapa kijijini rafiki zangu wote wameolewa, niliosoma nao wote wameolewa na wana miji yao, kila rafiki yangu ananiambia kuwa siwezi kuolewa kwakua nitamdarau mwanaume, Kaka mimi ni mtu wa kanisani, yaani kanisani wananidharau sana wanawake wenzangu.


Nikitaka kushiriki baadhi ya vitu wananiambia kwakua sijaolewa basi nisishiriki. Nipo kwenye kwaya nachangia hata safari lakini wananiambia kama sijaolewa bado sijaheshimishwa hivyo nitafute mwanaume wa kuniheshimisha. Kaka najaribu kutoa michango mingi ili angalau nionekane lakini sionekani.


Kaka nyumbani Mama nayeye kila siku ananiulizia kuhusu ndoa, kuna rafiki yangu anaolewa na Kaka mmoja ambaye wana mwezi tu Mama akanikasirikia. Mimi sikusoma kwakua Baba yangu alikua ni mlevi sana anampiga sana Mama yangu na hatuhudumii kwa chochote, nilianza Biashara ya kuuza nguo mnadani nikiwa na miaka 14.


Nina wadogo zangu wanne mimi ndiyo nawasomesha mmoja yupo chuo namlipia mimi na mwingine anaingia chuo mwaka huu, hao wadogo wapo sekondari ni mimi. Kaka natamani kuacha kila kitu ili niolewe, niliomaliza nao darasa la saba wote wana miji yao wana watoto wakubwa tu mimi peke yangu ndiyo sina mtu, nishauri Kaka.


NB: Kama una Matusi yako weka pembeni, huyu binti atasoma, nimeongea naye lakini ni kama haniamini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top