Mwanamke mwenye umri wa miaka 57 mkazi wa kata ya Puge wilaya ya Nzega mkoani Tabora ameuawa na kisha kuning'inizwa kwenye kamba ili aonekane amejinyonga mwenyewe.
Kituo cha redio cha CG FM kimeripoti tukio hilo ambapo kamanda wa polisi wa mkoa wa Tabora ACP SOPHIA JONGO amesema tukio hilo limetokea August 04 2021 katika kijiji cha Isalalo tarafa ya puge ambapo baba na mtoto wake wanatuhumiwa kuwa walimuua na kutengeneza tukio la kujinyonga