Mrembo mmoja amefanya harusi na picha ya mpenzi wake. Picha za hafla hiyo zilichapishwa kwenye kundi la Facebook, Igbo Rant HQ, na Vivian Chizoba.
Mrembo huyo asiyejulikana alikutana na jamaa huyo kwenye Facebook na walikubaliana kuoana baada ya kuzungumza kwa muda kupitia jumbe na simu. Jamaa huyo ambaye alidai kuwa na shughuli nyingi nje ya nchi, anaripotiwa kutuma pesa za harusi hiyo pamoja na picha yake akidai hangeliweza kuhudhuria.
SOMA HII AJINYONGA NA KUACHA WOSIA WA BARAKOA SONGWE
Katika picha zilizochapishwa, dada huyo anaonyeshwa akiwa amevalia mavazi ya harusi na kubeba picha ya mpenzi wake hafla nzima. Katika picha nyingine anaonyeshwa akiwa amesimama na maharusi na kushikilia picha ya mpenzi wake.
Hisia mseto
Anthony Enwere aliandika: "Inawezekana kwa sababu huenda jamaa hana stakabathi za kumrejesha nyumbani.Hivyo ndio vile anataka. Kuishi ng'ambo si rahisi. Mpangilio mrefu." Emmanuel Arome alisema:
"Ndio !! Inategemea na fikra zetu, ametuma vya kutosha, maoni yangu, iwapo ni ukweli au la alituma hizo mamilioni, kwa kweli, anaishi ughaibuni, huenda kazi yake haingelimruhusu, kwa hivyo ndoa ni kuelewana na kuaminana." Jane Ofili Igwe alisema:
"Hapana nilifikiri ni mazishi... Meza inakaa jeneza na picha yake juu. Hmmmmm." Marcel Amanda Adaora: "Msichana alitaka harusi na alipata.."
Jamaa afanya harusi na wake wawili siku moja Wakati huo huo,
mwanamume mmoja Mnigeria alikuwa amepanga kufunga pingu za maisha na wanawake wawili siku moja.
Picha ya kadi ya mwaliko ya harusi yake ilipakiwa kwenye Facebook na Emmanuel Gwatama, ambaye anadaiwa kuwa rafiki wa bwana harusi.
Akimtaja Kome kama shujaa wa mwaka, Emmanuel aliwahimiza wafuasi wake wa Facebook kuhudutia sherehe hiyo.
Bibi harusi kulingana na kadi hiyo walitambuliwa kama Maro na Akpove.
Harusi hiyo ya kitamaduni iliandaliwa Jumapili, Agosti 15, katika boma la marehemu Ekpe Hitler, mkabala na kituo cha Ugala Filing, Isoko Kusini jimbo la Delta.