CCM- UHURU WAPUUZWE KWA KWENDA KINYUME NA CCM

0

 Chama cha Mapinduzi kimesikitishwa na upotoshwaji mkubwa uliyofanywa na gazeti la Uhuru toleo Namba 24084 la leo Jumatano 11 Agosti, 2021, gazeti hili limepotosha sehemu ya mahojiano aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan na BBC.



Katika habari yake kuu limeandika kichwa cha habari “Sina wazo kuwania urais 2025- Samia” Huu ni upotoshwaji mkubwa na kumlisha maneno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.


Soma hii SHAKA;CHADEMA HAWAFANYI UTAFITI KUJUA KIPAUMBELE NI KATIBA AU UCHUMI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan hakusema kabisa maneno hayo, hili ni kosa kubwa linalokwenda kinyume na sera inayoongoza vyombo hivyo,  jambo ambalo halitavumiliwa hata kidogo  hivyo HATUA KALI za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika katika uandaaji wake.


Gazeti la Uhuru ndiyo “Adam na Hawa” wa magazeti yote hapa nchini, linawajibika kuonesha weledi wa hali ya juu na sio vinginevyo.


Tunawaomba Wanachama wa  Chama Cha Mapinduzi  na watanzania kwa ujumla kupuuza habari hiyo kwani imeandikwa na watu wenye maslahi yao binafsi. 


“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.  Samia Suluhu Hassan fikra na nguvu zake kwa sasa zimejikita  katika kuwatumikia watanzania na si vinginevyo” ——— Shaka Hamdu ShakaK-atibu wa Halmashauri Kuu ya CCM TaifaI,tikadi na Uenezi

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top